Fahamu maana ya ulipo mzoga ndipo watakapokutanika tai.

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom!, Nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo.

Maneno haya aliyazungumza Bwana Yesu kwa wanafunzi wako kuwaonya juu ya mambo yatakayotokea katika nyakati walizokuwepo baada ya yeye kuondoka lakini maneno hayo yanadhihirika kwa kasi ya ajabu hata kwetu sisi katika nyakati hizi za Mwisho hebu tusome.

Luka 17:22 “Akawaambia wanafunzi, Siku zitakuja mtakapotamani kuona siku moja katika siku zake Mwana wa Adamu, msiione.

23 Tena watawaambia, Tazama, kule! Tazama, huku! Msiondoke mahali mlipo, wala msiwafuate”;

Sasa kabla ya wanafunzi wake kumuuliza swali Bwana wetu Yesu Kristo kuna maneno yalitangulia kabla na ili tuweze kuelewa vyema tukisoma injili ya Mathayo imeeza kwa undani zaidi.

Mathayo 24:23 “Wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule msisadiki.

24 Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule.

25 Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele.

26 Basi wakiwaambia, Yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki”.

Unaona hapo!, Bwana Yesu aliwapa tahadhali wanafunzi wake katika nyakati za Mwisho akiwaonya wajihadhali kuwa wangi watakuja kwa jina lake na kila mmoja atakuwa akisema yeye ndie  Kristo ametoka kwa Mungu wamsikilize, wakiwadanganya tena kwa kufanya Ishara kubwa na miujiza mikubwa na watu wengi sana watadanganyika na kuona kweli Masihi yaani Kristo amerudi lakini sivyo.

Sasa Bwana Yesu alilijua hilo akatangulia kuwapa tahadhali kuwa watakapoona mambo kama hayo yakitukia wasidanganyike wal wasitishwe bali wabaki mahali pale pale walipo wasitoke kuwafata. Maana watawapotosha.

Sasa baada ya kusikia hayo wanafunzi wake wakabaki njia panda ndio ikabidi waulize Sasa wamuulize swali Bwana Yesu kwamba “NI WAPI SASA PATAKUWA SAHIHI AMBAPO HAPO HATUTAPOTEA TUTABAKI SALAMA?”

Bwana Yesu akawajibu swali walilouliza akawaambia “palipo na mzoga ndio watakapokusanyika tai” kwa maana nyingine mahali tai wanapokusanyika kula chakula chao ndipo wanapotakiwa kwenda wao!,
Kwa namna gani??

Sifa moja wapo ya hawa ndege wanaitwa Tai ni ndege wanaopaa juu sana kuliko ndege wengine wote, na wanapokuwa huko jicho la mwanadamu haliwezi kuwaona.

Lakini sifa nyingine kuu ni kwamba katika sehemu ambayo wewe huwezi kuwaona wao wanakuona vizuri kabisa yaani tai anasifa ya kuona mbali sana nje na upepo wa macho yetu!.

Hata unapotokea mzoga sehemu ambayo hakuna uwepo wowote wa ndege mfano jangwani ule mzoga unapokaa pale tai wanapokuwa kule juu wanauona na wanakuja kuula, utabaki kujiuliza mzoga ule umeliwa vipi wakati hakukuwa na dalili ya haya ndege mmoja angani na maeneo hayo wananyama kama ndege si rafiki kwao kukaa.

Hio ni kwa sababu tai wanaona chakula tokea mbali sana. Mahali ambapo sisi hatuwezi kuwaona.

Hio ikifunua Kristo pia  watu wake aliowakusudia toka kuwekwa kwa misingi ya ulimwengu amewapa jicho la tai la kuona fundisho la kweli liko wapi hata kama liko mbali na wao na limejificha vipi wataliona tu na watalifikia kwa njia yoyote ile ni lazima watalipata tu.

Hivyo hizi ni siku za Mwisho tuwe makini si kila chakula(fundisho ) kinatufaa vingine si vya kula ni sumu hivyo sio wakati wa kukurupukia mafundisho ya kila namna kisa tu yanafundishwa na mtu mashughuli anaekubalika na ulimwengu la!, tuwe Makini Kristo kashatuonya mapema.

Maranatha!.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>

https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *