Elewa tafsiri ya Mithali 20:1Mvinyo hudhihaki na kileo huleta ugomvi?

Maswali ya Biblia No Comments

Jibu: Turejee.

Mithali 20:1 “Mvinyo hudhihaki, kileo huleta ugomvi; Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima”.

Andiko hili linatupa ufahamu wa kuelewa kuna mambo makuu mawili yanayowakosesha watu waliopungukiwa na hekima, na Mambo Hayo tumeyaona hapo ni Mvinyo na kileo, vitu hivi vina madhara makubwa kwa mtumiaji yoyote..

Kuna tofauti kati ya kileo na mvinyo, na madhara yake kwa mtumiaji,”

Mvinyo Kwa lugha ya kingereza inajulikana kama wine, kilevi hiki kinatengenezwa kwa matunda yaliyosagwa kama maembe na nanasi, zabibu,

Na mfano mmojawapo wa mvinyo unaotengenezwa kwa matunda ni divai

Na huku kileo, ikijulikana kama beer/bia ,kilevi hiki kinatengenezwa kwa nafaka,mahindi,mtama,ngano na ulezi n.k..

Uhalisia Mvinyo ndio wenye kilevi kingi kuliko kileo, ingawaje matokea ya watumiaji wa hivi vyote yanakaribiana …

Madhara ya kutumia Mvinyo na kileo yapoje?

1.MVINYO

Maandiko yanasema Mvinyo hudhihaki, ikiwa na maana mtu anayetumia Mvinyo anakuwa ni mtu wa kudhihaki na kudhihakiwa kwa kuwa anatokwa na Maneno yasiyo na maana wala Heshima kinywani mwake..

Tunaona hata kipindi kile cha Pentekoste,walipowaona wanafunzi wa Bwana na kuwasikia wanasema kwa lugha waliwadhania wamelewa kwa mvinyo mpya na kuanza kutoa Maneno ya kuwadhihaki…

Matendo ya Mitume 2:12-16[12]Wakashangaa wote wakaingiwa na shaka, wakiambiana, Maana yake nini mambo haya?

[13]Wengine walidhihaki, wakisema, wamelewa kwa mvinyo mpya.

[14]Lakini Petro akasimama pamoja na wale kumi na mmoja, akapaza sauti yake, akawaambia, Enyi watu wa Uyahudi, na ninyi nyote mkaao Yerusalemu, lijueni jambo hili, mkasikilize maneno yangu.

[15]Sivyo mnavyodhani; watu hawa hawakulewa, kwa maana ni saa tatu ya mchana;

[16]lakini jambo hili ni lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yoeli,

Umepata kuona hapo, walianza kutoa Maneno ya dhihaka wakidhani wanafunzi wa Bwana wamelewa kwa mvinyo mpya,hii  ikituonyesha Siku zote Mvinyo unaleta dhihaka kwa anayetumia na ukilewa kwa mvinyo bado utapokea dhihaka nyingi…

2.KILEO

Biblia inazidi kutuonyesha, kwamba kileo huleta ugomvi, idadi ya watu wanaogombana mpaka kufikia hatua ya kudhuriana ni wanaokunywa pombe kupindukia, watu waliolewa kuna uwezekano wa kutokea mafarakano na mapigano..

Kwa kuhitimisha ni kuwa utumiaji wowote wa kileo au Mvinyo ni mbaya, kwasababu una matokea mabaya hata Katika ulimwengu tuliopo na ule unaokuja, Katika Neno la Mungu,walevi wote hawaturithi Ufalme wa Mungu, (soma 1Wakorintho 6:9-10 na Wagalatia 5:19-20)..

Warumi 13:13-14

[13]Kama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu.

[14]Bali mvaeni Bwana Yesu Kristo, wala msiuangalie mwili, hata kuwasha tamaa zake.

Maran atha..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *