Tafsiri ya Mithali 11:30 Mwenye hekima huvuta roho za watu

Maswali ya Biblia No Comments

Hapo maandiko yaliposema kuwa mwenye hekima huvuta roho za watu, ilimaanisha mtu yeyote anayewavuta watu katika wokovu huyo ndiyo anafahanishwa mtu mwenye hekima, hakumaanisha hekima za dunia hii maana hekima za dunia hii zipo nyingi lakini hazina faida kubwa kama hii ya mtu kumvuta mtu katika wokovu ..

Mithali 11:30 “Mazao ya mwenye haki ni mti wa uzima; Na mwenye hekima huvuta roho za watu”

Na jambo hili tunaliona kwa Bwana wetu Yesu Kristo, alikubari kuacha enzi yake na mamlaka huko mbinguni ili kuja kumkomboa mwanadamu, hiyo ni hekima kubwa sana kutafuta njia ya kumpatanisha mtu aliyekuwa amepoteza mahusiano na muumba wake kisha kupata kuaoata hekima ya kumrejeza ni jambo kubwa sana , hivyo hivyo bnasi ikiwa na sisi tumeshakwiaha kumwamini Yesu ya kuwa ni Bwana na mwokozi wa maisha yetu basi hatuna budi kumfuta Yesu aliye kielelezo chetu, nasi tutoke kukawalete watu kwa Yesu kuwapatanisha na Baba kama sisi tukivyo na mahusiano mazuri na BABA YETU, tujitoe pia kwa ndugu zetu ili nao wanaijue kweli iwaweke huru.

Sote tumepewa jukumu la kuhuburi injili, Hili jukumu si mchungaji, nabii, mtume nk…. Hapana bali ni la watu wote waliokikwisha kupokea neema ya wakovu, lazima tumzalie Mungu matunda.. ndipo hapo tutaonekana kama mwenye hekima.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *