fahamu maana ya mithali 30:24 Mjusi Hushika Kwa Mikono Yake; Lakini Yumo Majumbani Mwa Wafalme.

  Maswali ya Biblia

Tusome

Mithali 30:24-28
[24]Kuna viumbe vinne duniani vilivyo vidogo;
Lakini vina akili nyingi sana.
[25]Chungu ni watu wasio na nguvu;
Lakini hujiwekea chakula wakati wa hari.
[26]Wibari ni watu dhaifu;
Lakini hujifanyia nyumba katika miamba.
[27]Nzige hawana mfalme;
Lakini huenda wote pamoja vikosi vikosi.
[28]Mjusi hushika kwa mikono yake;
Lakini yumo majumbani mwa wafalme.

Mjusi ni kiumbe ambaye ni tofauti sana na viumbe wengine, kwa namna Mungu alivyo muumba anao uwezo wa kupita sehemu yoyote hata kuwe na upenyo mdogo lazima atapita tu, wakati mwingine kupitia mikono yake anao uwezo wa kisimama katika pembe yeyote ya ukuta iwe pembeni au juu anaweza kukaa mahali pale pasipo kudondoka, wapi tafaiti sana na wanyama wengine ambao wao ili waweze kupanda mahali pa juu lazima watumie kucha zao kupanda.

Na kiuhalisi wapo kila nyumba, yaani nyumba yeyote ile huwezi kuwakosa lazima tu watakuwepo hata nyumba iwe na ulinzi kiasi gani lazima itawakuta tu maana wao wao huingia mahali popote na kukaa, ndiyo maana katika kifungu hicho ” Mjusi hushika kwa mikono yake;
Lakini yumo majumbani mwa wafalme.” Umeona hapo japo hushika kwa mikono lakini hata katika majumba ya wafalme, maraisi lazima tu utawaona na wanakaa pasipo shida yeyote ..

Inafunua nini rohoni hekima hii ya kiumbe hiki, katika maisha yetu?

Ikiwa na sisi tutamwamini Yesu Kristo maishani mwetu, huu uwezo wa kuingia mahali popote tutakuwa nao, tunaweza kuingia hata katika sehemu ambazo zinaonekana haziwezekaniki kuingia sisi tuweza kuingia, hata katika malango ya adui aliyozuia tukiwa ndani ya Kristo huko kote tunakwenda na kuaharibu bila shida kabisa
Lakini kama tukiwa mbali na Bwana wetu Yesu, yaani hatujamwamini ni ngumu sana kuweza kuingia mahali ambapo pamezuiliwa na mwovu ni ngumu sana ndipo hapo unatakuata unapitia kipindi kigumu kwa sababu umekosa uwezo wa kwenda kupanigia mahali fulani au unaona wokovu mgumu nk hayo yote huwa yanaonekana magumu endapo tu unakuwa nje ya Kristo

Mwanzo 22:17 “katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; NA UZAO WAKO UTAMILIKI MLANGO WA ADUI ZAO;
18 na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu”

Kwa kumkiri kwako Kristo utaona vifungo vingi vimeashia na yale ambayo ulikuwa huyawezi kuyandea basi utashangaa unaweza nini wewe tu kumwamini Yesu Awe Bwana na mwokozi wa maisha yako, hapana Mwokozi mwingine tofauti na BWANA WETU YESU KRISTO..

SHALOM

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT