MASUKE NI NINI?

Maswali ya Biblia No Comments

MASUKE NI NINI?

Masuke ni ile sehemu ya nafaka inayotoa ua na mbegu ndani yake, Kwamfano Ngano suke lake linachipuka kwa pale juu, na nafaka kama mahindi suke lake ndio lile linalochipukia hindi lenyewe. Lakini nafaka yote sio suke, wala hindi lote sio suke, bali ile sehemu inayotoa mbegu au ua au tunda ndio inaitwa suke

Hivyo zamani, kama mtu akitaka kula ngano iliyo mbichi, ambayo kiafya ilikuwa haina shida, kwani jamii za watu wa mashariki ya kati kama vile wapalestina na waarab, zamani na hata sasa, wanaoutarabu huo wa kula, nafaka mbichi, hususani ngano ambayo haijapikwa..

Ndiyo maana jambo hili Mungu aliliruhusu Kwa watu wa agano la kale pindi pale mtu atakapo hisi njaa, na akawa amepita karibu na shamba la mtu mwingine, basi anaruhusa ya kula suke pale pale lakini asivune

tunasoma hili katika
Kumbukumbu 23:25 “Uingiapo katika mmea wa jirani yako waweza kuyapurura masuke kwa mkono wako; ila usisongeze mundu katika mmea wa jirani yako”.

katika agano jipya tunaona tena jambo hili linatajwa tusome

Luka 6:1 “Ikawa siku ya sabato moja alikuwa akipita katika mashamba, wanafunzi wake wakawa wakivunja masuke na kuyala, wakiyapukusa-pukusa mikononi mwao”.

Katika habari hii tunaona Yesu akiwa na wanafunzi, wakati wapo njiani wanafunzi wake walishikwa na njaa,
na mahali walipokuwa wanapitia walikuwa karibu na shamba waliingia na kuanza kuvunja masuke na kula, lakini hiyo siku ilikuwa siku ya sabato

Na mafarisayo walipoona wakaanza kuwashutumu kuwa wanaihalifu sabato kwa wanachokifanya, ndipo Bwana Yesu akawaeleza habari ya alichofanya Daudi alipokuwa na njaa jinsi alivyokula ile mikate ya wonyesho ambayo sio sahihi yeye kuila bali makuhani tu peke yao.

Na mwisho kabisa akawaambia mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato.

Tunajifunza Nini nasi katika habari hii
Je nasi ni sawa Leo hii kama tukishikwa na njaa tuingie kwenye shamba la mtu na kuanza kula bila ruhusa yake, mfano shamba la miwa , ndizi, machungwa nk..
kulingana na hicho kifungu

Lazima tuelewa kuwa agizo hilo lilitolewa kwa wana wa Israeli kama taifa, hivyo ilijulikana na watu wote ndiyo maana haikuwa shida watu kufanya hivyo endapo wanapapotwa na njaa

Ila sisi wamataifa kumbuka tunaishi na watu tofauti tofauti Kila mtu ana tabia yake, haswa tunaishi pia na watu wasio mcha Mungu

Lazima tuwe na hekima katika kuishi kwetu na kuenenda kwetu ili tusilete madhara, mfano ukikutana na mtu ambaye hana huruma ni rahisi kukuharibu ambaye umeingi katika shamba lake bila Ruhusa yake..

Bwana akubariki
Kwa Maswali, Maombezi, au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi Kwa namba hizo
+225693036618/ +225789001312

Pia jiunge na channel yetu ili uweze kufikiwa na masomo mbali mbali

NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *