ARABUNI ni nini?

  Biblia kwa kina

Katika Agano la Kale arabuni imetajwa mara nyingi zaidi. Hivyo Arabuni ni Eneo ama sehemu ambayo iko mashariki ya kati.

Ampapo wafanyabiashara mbali mbali walikuwa wakimletea Fedha, dhahabu nk Mfalme Sulemani

2Nyakati 9:14 “mbali na ile waliyoileta wachuuzi na wafanya biashara; tena wafalme wote wa Arabuni, na maliwali wa nchi wakamletea Sulemani dhahabu na fedha”.

Hivyo katika sehemu hii kulikuwa na nchi nyingi, Arabuni hakukuwa na nchi moja tu bali zilikuwa ni nyingi tunalidhibitisha hilo tukisoma. “2 Nyakati 9:14……wafalme wote wa Arabuni…….”

Biblia katika Agano la Kale imetaja katika sehemu nyingi neno hili Arabuni.

Yeremia 25: 13 “Ufunuo juu ya Arabuni. Ndani ya msitu wa Arabuni mtalala, Enyi misafara ya Wadedani”.

Katika Agano Jipya pia Neno hili limetajwa mara kadhaaa na linamaanisha jambo lingine tofauti kabisa na agano lile la Kale.

Arabuni katika agano la Kale ilikuwa ni sehemu yaani ni jambo la mwilini lakini katika agano letu jipya Arabuni ni jambo la rohoni.

Arabuni ya roho nayo si nyingine zaidi ya Roho Mtakatifu. Hivyo Roho Mtakatifu ndio Arabuni yetu yaani ni zawadi ambayo Mungu ametupa ili kutuwezesha katika mambo mbali mbali tusiyoyaweza hata tutanye nini.

Sasa Arabuni hii ni kama “ENTRANCE ” yaani maingilio. Au tunaweza kusema ni guarantee yaani hakikisho.

Mungu ametupa sisi uzima wa milele baada ya akumpokea Kristo Yesu kuwa ni Bwana na Mwokozi wetu, hivyo hajatuacha hivi hivi tu bali katuba Roho wake ili kutupa hakikisho ndani yetu kuwa uzima huo hakika tunao.

2Wakorintho 1:22 “naye ndiye aliyetutia muhuri akatupa arabuni ya Roho mioyoni mwetu”.

Mhuri unaozungumziwa hapa ni Roho Mtakatifu ndie anatutambulisha sisi kuwa ni watoto wa Mungu.

Tunalidhibitisha hilo tukisoma..

Waefeso 1:3 “Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na

Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu.14 Ndiye aliye arabuni ya urithi wetu, ili kuleta ukombozi wa milki yake, kuwa sifa ya utukufu wake”

Hivyo ukipokea Roho Mtakatifu inakupa hakikisho kuwa wewe ni Mwana wa Mungu, wala hakuna laana, magonjwa,Uchawi juu yako.

Pia utaweza kuomba katika Roho na kweli na maombi yako ni hakika yanafika kwa Mungu maana Roho pia hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.

Warumi 8:26″Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.”

Hivyo ni Faida nyingi tunapopata Arabuni hii ya thamani kutoka kwa Mungu yaani Roho Mtakatifu kwani pia hutusaidia kuomba HALELUYA HALELUYA.

Lakini usipokuwa na hii Arabuni ya roho yaani Roho Mtakatifu maana yake kuwa wewe si wake maana maandiko yanatwambia wazi kabisa.

Warumi 8:9 “…Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake”.

Maana pasipo yeye huwezi kuishi maisha makamilifu na si hivyo tu huwezi poa pia kuwa ni mrithi wa ahadi za Mungu.

Je!, umeokoka? Umepokea Roho Mtakatifu? Ufanyike kuwa mwana na Mrithi wa ahadi za Mungu? Kama bado hujaokoka nafasi unayo bado sasa maadamu giza bado halijaja, fungua moyo wako sasa umpoke Yesu upate Arabuni ama guarantee (hakikisho) ndani yako.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine.

Kwa msaada zaidi wasiliana nasi +255 789001312.

NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

LEAVE A COMMENT