Mchuuzi ni mtu wa namna gani kibiblia?

Maswali ya Biblia No Comments

Bwana Yesu Kristo Asifiwe. Nikukaribishe tujifunze maneno ya Uzima

JIBU:


Hosea 12:7
“NI MCHUUZI, mizani ya udanganyifu i mkononi mwake; anapenda kudhulumu .”

Mchuuzi ni mtu anayejishughulisha na ununuaji wa bidhaa na kuzisafirisha kuziuza sehemu nyingine hususani nje ya nchi yake.


Unaweza kupitia tena, utalipata katika Wimbo ulio Bora 3:6, Ezekiel 27:3, 27:20-22 pamoja na Isaya 23:8

JE? Biblia inaruhusu Wakristo kuwa Wachuuzi ?

Ndio inaruhusu!. Isipokuwa katika biashara yoyote hakikisha mkristro unazingatia Viwango vya utakatifu na Ukamilifu. Uchuuzi unapohusisha masuala ya udhalimu, Rushwa, Mambo haramu n.k ni hatari kwa mwamini kama ilivyoandikwa katika..

Ezekieli 28:18-19
18 “Kwa wingi wa maovu yako, katika uovu wa uchuuzi wako, umepatia unajisi patakatifu pako; basi nimetokeza moto kutoka ndani yako, nao umekuteketeza, nami nimekufanya kuwa majivu juu ya nchi, machoni pa watu wote wakutazamao.

19 Wote wakujuao kati ya kabila za watu watakustaajabia; umekuwa kitu cha kutisha, wala hutakuwapo tena hata milele.”

UBARIKIWE

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *