Mjoli ni nani katika biblia?

Maswali ya Biblia No Comments

Karibu tujifunze neno la Mungu wetu.

Mjoli ni mfanyakazi mwenza, mfano Mwana kwaya akikutana na mwanakwaya mwenzake hapo ni sawa na kusema kakutana na mjoli mwenzake, vivyo hivyo Mwalimu akikutana na Mwalimu mwenzake hapo kakutana na mjoli wake, Mkulima akikutana na mkulima mwenzake hapo Mkulima ni sawa tu na kusema kakutana na mjoli wake.

Hivyo wajoli au mjoli ni watu wanaofanya kitu kimoja kinachofanana , mhubiri kwa mhubiri ni wajoli pia.

Tusome..
Wafilipi 4:3
Naam, nataka na wewe pia, MJOLI wa kweli, uwasaidie wanawake hao; kwa maana waliishindania Injili pamoja nami, na Klementi naye, na wale wengine waliotenda kazi pamoja nami, ambao majina yao yamo katika kitabu cha uzima.

Tusome pia..
Mathayo 18:23-35
[23] Kwa sababu hii ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyetaka kufanya hesabu na watumwa wake.

[24] Alipoanza kuifanya, aliletewa mtu mmoja awiwaye talanta elfu kumi.

[25] Naye alipokosa cha kulipa, bwana wake akaamuru auzwe, yeye na mkewe na watoto wake, na vitu vyote alivyo navyo, ikalipwe ile deni..

[26] Basi yule mtumwa akaanguka, akamsujudia akisema, Bwana, nivumilie, nami nitakulipa yote pia..

[27] Bwana wa mtumwa yule akamhurumia, akamfungua, akamsamehe ile deni.

[28] Mtumwa yule akatoka, akamwoma mmoja wa WAJOLI wake, aliyemwia dinari mia akamkamata, akamshika koo, akisema Nilipe uwiwacho.

[29] Basi mjoli wake akaanguka miguuni pake, akamsihi, akisema, Nivumilie, nami nitakulipa yote pia.

[30] Lakini hakutaka, akaenda, akamtupa kifungoni, hata atakapoilipa ile deni.

[31] Basi WAJOLI wake walipoyaona yaliyotendeka, walisikitika sana, wakaenda wakamweleza bwana wao yote yaliyotendeka.

[32] Ndipo bwana wake akamwita, akamwambia, Ewe mtumwa mwovu, nalikusamehe wewe deni ile yote uliponisi;

[33] nawe, je! Haikukupasa kumrehemu MJOLI wako, kama mimi nilivyo kumrehemu wewe?

[34] Bwana wake akaghadhibika , akampeleka kwa watesaji, hata atakapoilipa deni ile yote.

[35] Ndivyo na Baba yenu wa mbinguni atakavyowatendea ninyi, msiposamehe kwa mioyo yenu kila mtu na ndugu yake.

Vifungu vingine, soma pia ..Ufunuo 22:9, 19:10, Wakolosai 4:7, 1:7.
_
Hivyo na watakatifu wote ulimwenguni kote, tuliookolewa na Yesu kristo, kila mmoja ni mjoli kwa mwenzake.

Je! na wewe umefanyika mjoli pamoja na watakatifu wa Mungu? Kumbuka biblia inasema katika waebrania 12:14 hapana mtu atakaye mwona Mungu pasipo utakatifu.

Hivyo kama bado ujamwamini Yesu kristo, wakati ni sasa, mlango wa Neema bado haujafungwa, Tubu dhambi zako, kisha ukabatizwe ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu kristo. Matendo ya mitume 2:37-38.

Bwana akubariki.

Kwa msaada waweza kuwasiliana nasi Kwa namba hizi
+225789001312/ +2256930306618

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *