Neema ni nini?

  Maswali ya Biblia

Shalom, karibu tutafakari Maneno ya Uzima wetu…

Neema tafsiri halisi ni upendeleo usiokuwa na sababu yoyote, au kupata kukubaliwa kusikostaili, na Kiuhalisia kuna upendeleo ulio na sababu na usio na sababu, mfano hai wa upendeleo ulio na sababu ni wa sisi wanadamu,ambao tunapendana na kujaliana walio wetu, wale tunaowafahamu na wenye faida kwetu,..

Si rahisi kwa mwanadamu yoyote kumpa upendeleo mtu ambaye ni adui yake, au kutoa upendeleo kwa mtu anayemuudhi,anayeweza kufanya hayo yote ni Mungu peke yake, Mungu mwenyewe ndiye mwenye uwezo wa kumpa upendeleo yule ambaye hastahili kitu..

Tusome hapa ili tuzidi kuielewa  Neema

Mathayo 20:9-16[9]Na walipokuja wale wa saa kumi na moja, walipokea kila mtu dinari.

[10]Na wale wa kwanza walipokuja, walidhani kwamba watapokea zaidi; na hao pia wakapokea kila mtu dinari.

[11]Basi wakiisha kuipokea, wakamnung’unikia mwenye nyumba,

[12]wakisema, Hao wa mwisho wametenda kazi saa moja tu, nawe umewasawazisha na sisi tuliostahimili taabu na hari za mchana kutwa.

[13]Naye akamjibu mmoja wao, akamwambia, Rafiki, sikudhulumu; hukupatana nami kwa dinari?

[14]Chukua iliyo yako, uende zako; napenda kumpa huyu wa mwisho sawa na wewe.

[15]Si halali yangu kutumia vilivyo vyangu kama nipendavyo? Au jicho lako limekuwa ovu kwa sababu ya mimi kuwa mwema?

[16]Vivyo hivyo wa mwisho watakuwa wa kwanza, na wa kwanza watakuwa wa

mwisho.

Umepata kuona hapo, kwamba wale waliofanya kazi kutwa nzima wamelipwa sawa tu na wale waliofanya kazi lisaa, ni upendeleo alioufanya huyu mwenye kuajiri,ni vile amewapendelea, kwasababu hakukuwa na sababu iliyowafanya walipwe sawa na wale waliotaabika ,tena ingewapasa wapate malipo kidogo zaidi ya wengine na walipaswa kupata malipo mwisho kabisa lakini tunaona wao ndio waliokuwa wakwanza kulipwa,hii ndio tunaitafsiri mfano wa NEEMA 

Tukitazama kimaandiko tunaona ipo Neema moja iliyo kubwa ambayo tumepewa sisi wanadamu, na si nyingine zaidi ya UZIMA WA MILELE, tunaona baada ya kuanguka kwa wazazi wetu wa kwanza pale edeni, Kiuhalisia hatukustaili tuwe na nafasi ya kuishi milele, kwasababu kutokana na anguko stori yetu ingeishia hapo hapo, labda ingempendeza Mungu kuumba viumbe wengine,hatujui ila kwa upande wetu ingetakiwa habari zetu ziishie pale pale..

Lakini tunaona pendo la Mungu la kutupenda likavuka mipaka pasipo kuwa na sababu yoyote,tunaiita bahati,ikampendeza kutupa Uzima wa milele, wala si kwakuwa tulikuwa na sura za huruma mbele za Mungu kwamba ndio sababu ya kutupa Uzima wa milele,sivyo, na si kwasababu tulimwomba au kuomba sana…Ni Neem yake tu,Ni Neema…

Tusidhani kulikuwa na sababu Mungu kutupa Uzima wa milele au kutupoteza kungemfanya Mungu kuona ni kitu kikubwa kwake, mamiaka yasiyo hesabika huko nyuma alikwepo tena pasipo sisi, hivyo tusijione tuna uthamani sana mbel e za Mungu iliyopelekea kutupa sisi uzima wa milele,Ni Neema yake tu,alikuwa na uwezo wa kufuta kila kitu akaumba kitu kingine na kutusahau kabisa sisi..Ni Neema

Na tunafahamu mpango wa Wokovu ulishuka kwa kumtuma Mwanae mpendwa,YESU KRISTO ambaye kila atakayemwamini huyo atapata Uzima wa milele..

Yohana 1:14  “Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; AMEJAA NEEMA NA KWELI”.

Ikiwa leo utatafakari Neema ,kwa Wokovu tulioupata ambao hatukustaili kabisa unapataje ujasiri wa kuudharau huu msalaba wa Yesu?

Maaandiko yanasema..

Waebrania 2:3  “sisi je! Tutapataje kupona, TUSIPOJALI WOKOVU MKUU NAMNA HII? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia”.

Huu sio wakati wa kuidharau hii Neema ya Mungu, kwasababu huko ndiko ghadhabu ya Mungu ilipofichwa, kwa kuwa siku ikiondoka Neema ndipo tutakuja kufahamu hatukuwa watu maalumu, na tutaelewa kuwa Mungu anaweza kuendelea kuishi bila hata sisi wanadamu..

Waebrania 10:28-29[28]Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu.

[29]Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?

Ndugu yangu ,tuko mwisho kabisa wa hii Neema tunaoichezea,fahamu kabisa hii Neema haitadumu milele, parapanda itakapolia ndipo Neema hii itafika ukomo wake,na wale watakaobaki kwenye unyakuo ndio watakao kuwa na  uhakiki wa hii Neema, vile watakapokuwa kwenye mateso makali,maumivu kwa kulia katika ziwa la moto ndipo watakapofahamu hisia zao haziwezi kuwa kitu mbele za Mungu, wataona kuwa hatukuwa maalumu sana kama tulivyokuwa tunahubiriwa ndipo wataelewa waliichezea Neema ya Mungu..

Mimi na wewe tusiwe watu tutakaokaa na kutengwa na Neema ya Mungu milele, Mpokee Yesu Kristo ili usipoteze hii Neema..

Shalom…

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT