Nini maana ya Mithali 28:8 “Yeye azidishaye mali yake kwa riba na faida, Humkusanyia mtu awahurumiaye maskini,

Maswali ya Biblia No Comments

Mithali 28:8[8]Yeye azidishaye mali yake kwa riba na faida, Humkusanyia mtu awahurumiaye maskini..

Hapo biblia imemzungumzia mtu anakuyekusanya mali zake kwa  faida na  riba, ni yule mtu anayejipatia mali kwa njia ambazo hazina uhalali wowote na kuwadhulumu walio katika hali ya chini/ wanyonge…

Katika biblia kipindi cha wana wa Israel,Mungu aliwapa agizo wasiwatoze riba pindi watakapowakopesha, na  tena wasichukue faida kutoka kwa ndugu zao yaani (waisraeli kwa waisraeli) zaidi wafanye hayo kwa watu wageni, watu wa taifa lingine..

Kutoka 22:25
[25]Ukimkopesha mtu aliye maskini, katika watu wangu walio pamoja nawe; usiwe kwake mfano wa mwenye kumdai; wala hutamwandikia faida.

Pitia tena Walawi 25: 35-37, kumb 23

Lakini kulikuwa na idadi kubwa ya matajiri walioenda kinyume na agizo hili la Mungu na kufanikiwa huko kukaongeza idadi kubwa ya mali zao za kujilimbukizia na kuwa kama mavumbi..

Ayubu 27:13-16[13]Hii ndiyo sehemu ya mtu mwovu kwa Mungu, Na urithi wa hao waoneao, waupokeao kwa Mwenyezi.

[14]Watoto wake wakiongezeka ni kwa upanga; Na wazao wake hawatashiba chakula.

[15]Hao watakaosalia kwake watazikwa katika kufa, Wala wajane wake waliofiwa na waume hawataomboleza.

[16]Ajapokusanya fedha kama mavumbi, Na kujifanyia mavazi kama udongo kwa

wingi;

Zaidi maandiko imetoa pia hitimisho ya watu kama hawa,maana mwisho wao ni Mungu kuwapokonya na kuwapa wenye kuweza kutenda mema kwa kuwahurumia wenye uhitaji na masikini..

Jambo hili linawezekana, kwasababu, biblia inasema mali ina mbawa, inaweza ikaondoka na kupaa gafla, au ukashangaa imeingia Katika Matumizi yasiyo na umuhimu na ikapuputika yote, au ikafika muda wako ukafa ukawa haupo na mali yako akachukua mwingine, na kule mali yako inapokwenda fahamu inakwenda mahali salama,mahali ambapo ataipata mtu atakayewajali watu wa hali za chini..

Ni kweli kabisa Mungu anaweza kufanya hivyo..

Usipoweza kuitumia talanta yako vema,anasema mnyang’anyeni mwenye moja mkampe mwenye kumi (Mathayo 25:28),usipojua kukitumia kama ipasavyo, Bwana anauwezo wa kukunyang’anya..

HILI LINATUFUNDISHA NINI?

Tukipenda kuwa watu wa kutenda haki,na kuwahurumia wenye uhitaji na masikini,tutaingia kwenye daraja ambalo litakuwa ni Mungu kuandaa hazina zitokazo kwa watu waovu,waliofanya dhuluma na kujiwekea fedha kwenye account zao za benki na wala hawakutumia njia halali Katika mambo yao..

Jambo hili linatuonyesha jinsi gani tukiwa na tabia ya kupenda kusaidia wengine na kuwapa vitu tunajiweka kwenye daraja zuri na kuwa na hazina kubwa duniani..

Kwa Neema za Bwana atusaidie tuweze kuifahamu hekima hii,tuweze kutoa msaada kwa wengine…

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *