Mithali 24:17,ina maana gani kusema, tengeneza kazi yako huko nje?

  Maswali ya Biblia

JIBU..

Mithali 24:27[27]Tengeneza kazi yako huko nje, Jifanyizie kazi yako tayari shambani, Ukiisha, jenga nyumba yako..

Wakati wa zamani, Katika biblia kilimo kilikuwa na nafasi kubwa sana kwa watu,tunaweza kusema kilikuwa ni uti wa mgongo kama ilivyo leo katika nyakati zetu kwenye baadhi ya jamii mbalimbali…

Na ilikuwa ni jambo la kushangaza kwa kipindi hicho mtu kuchukua baadhi ya rasiminali zake na kwenda kufanyia manunuzi fulani, labda ni wanyama, nyumba n.k,ikiwa Katika mashamba yake hajajiwekeza vizuri..

Ilikuwa ni desturi yao kujiwekea hazina za kutosha kwanza za vyakula Katika maghala yao kwa miezi au miaka kadhaa, baada ya hapo ndipo huanza kufikiri na kupanga ni namna gani wanaweza kujiendeleza kwa kujenga na kufanya mambo mengine,na hawakujiendeleza kwanza bali walihakikisha mashamba yao yanawanufaisha na kuwaletea faida..

Na hapo ndipo mfalme Suleiman anazungumzia jambo Hilo..

Mithali 24:27
[27]Tengeneza kazi yako huko nje,
Jifanyizie kazi yako tayari shambani,
Ukiisha, jenga nyumba yako.

Kwa lugha nyepesi tunaweza kusema,ni wewe kuweka mambo yako kuwa imara kwanza, ndipo yale mengine yawe ya ziada, au yafuate badae..

Ni kawaida ya wanadamu kupenda vitu vinavyotamanika,au vitu vizuri kabla hajavitaabikia wala kuvisumbukia..

Tunamwona mtumwa mmoja wa Nabii Elisha,aliyeitwa Gehazi,yeye hakuifahamu hii kanuni,akaona kuzisubiri baraka za Bwana ni kama kuchelewa, kutumika mbele ya bwana wake ni kupoteza muda, hivyo wakati Naamani amemletea Elisha zawadi zenye thamani nyingi na Elisha kuzikataa,akaona kama Elisha hapendi yaliyo mema, ndipo tunaona nabii Elisha anamwambia…

2 Wafalme 5:26[26]Akamwambia, Je! Moyo wangu haukuenda na wewe, hapo alipogeuka yule mtu katika gari ili akulaki? Je! Huu ndio wakati wa kupokea fedha, na kupokea mavazi, na mashamba ya mizeituni, na mizabibu, na kondoo, na ng’ombe, na watumwa, na wajakazi?

Umeona hapo,amemuuliza,Je huu ndo wakati?

Ukiangalia kumbe kulikuwa na wakati wake lakini si ule..

Watu wa leo wanataka kuona wanapokea baraka za Mungu bila kutaka kutengeneza kwanza Katika mashamba yao,hawana muda na kazi ya Mungu, kuhubiri kwao ni ngumu,kilicho Katika fikra zao ni wale vizuri,matumbo yao yashibe..kibaya zaidi wanaendelea kufikiri kwamba kuna faida gani watapata..

1 Timotheo 6:5-6[5]na majadiliano ya watu walioharibika akili zao, walioikosa kweli, huku wakidhani ya kuwa utauwa ni njia ya kupata faida.

[6]Walakini utauwa pamoja na kuridhika ni faida kubwa

Wakati mwingine hekima za ulimwengu zina maana,unapofikiri kununua simu ya milioni tatu na huku huna shughuli yoyote ya kufanya,ni heri ukaitumia hiyo milioni tatu kufanya biashara ili iendelee kukuongezea faida ya kununua simu..

Ni Bwana Yesu pekee anayeweza kuyapangilia maisha yetu ya rohoni na Mwilini, mpokee Leo maishani mwako..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT