maana ya Yesu kuitwa mwana wa Azali?

  Maswali ya Biblia

Maana ya neno Azali ni “MILELE” yaani kitu kisichokuwa na mwanzo wala mwisho.

Hivyo Yesu kuitwa Mwana wa Azali inamaanisha Yesu ni Mwana wa Mungu asiye kuwa na mwanzo wala mwisho.

SWALI: Ni kweli Yesu ni Mwana wa Azali?

Ndiyo ni kweli, Yesu ni Mwana wa Azali Kwa sababu yeye ni mwana wa Mungu maandiko yamelithibitisha jambo hili tusome

Waebrania 7

1 Kwa maana Melkizedeki huyo, mfalme wa Salemu, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu alipokuwa akirudi katika kuwapiga hao wafalme, akambariki;

2 ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, tena, mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani;

3 hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele.

Yesu alivaa umbile la kibinadamu ili kutukomboa, lakini yeye ni ndiyo Mfalme wa Amani, yeye ndiye Yehova Elohimu hii ni ofisi tu ya kutendaji kazi wake lakini yeye ni Mwanzo na Mwisho yaani ni Mungu mwenyewe, ambaye alikuwa kwetu Kwa umbile la kibinadamu ili apate kutupa wokovu tuliopoteza hapo mwanzo uliopotezwa na wazazi wetu wa kwanza ni ofisi ambayo ilifanya upatanisho.

2 Wakorintho 5

18 Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, naye alitupa huduma ya upatanisho;

19 yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho.

Kwahiyo Neno Azali ni Mungu mwenyewe, MUNGU KWELI KWELI HANA MWANZO WALA MWISHO, MUNGU MUUMBA WA MBINGU NA NCHI ambaye alikubali kuacha enzi yake mbinguni akaja kumkomboa mwanadamu ili asipotee bali awe na uzima wa Milele.

Mungu aliacha enzi ili aje akukupe leo uzima wa milele uondokane na hukumu inayokuja, ambayo Mungu atamlipa mtu sawa sawa na alichokifanya akiwa hapa dunia, Je umempokea Yesu Kristo maisha mwako sawa sawa na (warumi 10:9) Je umeokoka, tazama ni Pendo la ajabu ambalo Mungu amekupa Leo amekupa njia ya kukuokoa wewe ili usipotee, ili siku hiyo utakapo fika uwe uwe na amani, lakini ukiipuuzia jambo hili Je ile siku utamwambia nini Mungu ukimwona Kwa kushindwa kutii Neno lake, amekupa nafasi tena ya kipekee, kumbuka hakuna njia nyingine ya kumwona Mungu tofauti na Yesu Kristo hivyo ukipokea Kristo umepata njia ya kwenda mbingu

Yohana 14

6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.

7 Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona.

Ikiwa bado ujaweka maisha yako sawa basi Mwamini Leo Mwana Azali maana alishuka dunia ili sisi tupone..

ubarikiwe

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT