Maana ya Maziwa ya akili yasiyoghoshiwa ni nini? (1Petro 2:1-2)

Maswali ya Biblia No Comments

1 Petro 2:1-2[1]Basi, wekeni mbali uovu wote na hila yote, na unafiki na husuda na masingizio yote.

[2]Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;

Neno kughoshi lina maana ya kugeuza, au kutia kitu dosari, na lengo lake ni kukifanya kitu kionekane kama kile cha kwanza,ndo mana utasikia watu wakisema vyeti vimeghoshiwa, akimaanisha kuwa wamefanya ubadilifu kwa kutengeneza vyeti bandia ili kuonekana kama wamehitimu kumbe kuna uongo..

Mfano mwingine wa watu wanaogoshi fedha, maana yake wanatengeneza fedha bandia ili ziweze kuonekana kama zina uhalisia wa fedha halali kumbe sivyo,na lengo lao zitumike kwa Matumizi…

Mtume Petro alizungumzia  hapo, kwamba tuyatamani maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, alifananisha na maziwa wanayonyonya watoto wa wachanga na Neno la Mungu, kwasababu maziwa wanayonya Watoto kutoka Moja kwa moja kwa mama zao huwa hayajagoshiwa wala kutiwa kitu kingine, Mtoto anakuwa anayanyonya moja kwa moja kwa mama yake…

Ukiangalia kwa  kipindi cha leo mambo yamekuwa ni tofauti, Watoto wamekuwa hawanyonyi wala kuyapata maziwa yaanayotoka kwa mama zao,bali wamekuwa wakitafutiwa njia mbadala kutoka kwenye maziwa yanayohifadhiwa kwenye makopo,au kwa wanyama kama ng’ombe, kwa kuwa ukiyatazama yanafanana na maziwa ya mama, lakini ukweli ni kwamba yapo mbali Katika ubora na Katika Afya ya Mtoto..hayo yanayohifadhiwa kwenye makopo asili yake kubwa yana kemikali ambayo inafanya yasiharibike bali yatumike kwa muda mrefu, haya ndo tunayaita maziwa yaliyogoshiwa ambayo yanakuwa mbadala wa maziwa ya mama lakini hayawezi kuwa na ubora kama wa Yale ya mama…

Hivyo vivyo na walio Wakristo tunahitajika kuyanyonya maziwa yanayotoka moja kwa moja kwa Mungu wetu,yanayotoka Katika Maaandiko Matakatifu,(yaani BIBLIA) haya ndo maziwa yetu,matiti yetu ili tukue  katika Wokovu na kumpendeza Mungu,na kuwa na Afya njema ya kiroho njia ni kulifyonza Neno lake Maishani mwetu..

Lakini tukichukua injili nyingine na kuifanya msingi wa maisha yetu basi tujue tunajidhoofisha wenyewe..

Utajiuliza ni kwanini wakristo wengi wanashindwa kudumu katika Wokovu,leo kasimama lakini Kesho kaanguka Katika dhambi, mwingine yupo Katika imani kwa kipindi kirefu,yupo kwenye kanisa lakini hana matunda yoyote kwa Mungu, ukiangalia ni wangapi aliwahubiria habari njema,hakuna, sasa hayo yote yanasababishwa na kunywa maziwa mengine yasiyokutia nguvu za rohoni..

Upo sehemu lakini injili unayohubiriwa ni ya mafanikio tu,sio utakatifu na siku za Mwisho,hukemewi dhambi zako kwamba ni Machukizo kwa Mungu,fahamu hayo ni maziwa yaliyogoshiwa ambayo yanafanana na yale halisi,hayo hayatakusaidia chochote Katika kuushinda ulimwengu…

Msisitizo wa Mtume Paulo ni sisi, Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa tuyatamani maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu’

Hatuna budi kuitafuta kwa bidii na kuitamani injili ya Kweli, injili iliyoandikwa na mababa zetu,ambao ni Mitume, ili tuweze kuushinda ulimwengu na mwovu shetani, na kuukulia Wokovu wetu Katika kuyafanya mapenzi yake Mungu Kwa kumzalia matunda..

Tukumbuke hizi ni nyakati za mwisho, Mafundisho na injili nyingi za uwongo zimesambaa kila kona, Ndio maana Bwana Yesu alituhadharisha mapema kwamba ANGALIE JINSI MSIKIAVYO (Luka 8:18)…akimaanisha tuwe makini na yale yanayohubiriwa kwasababu sio Yote yanayojenga roho zetu, mengi ya hayo ni feki,yamejaa udanganyifu mbaya wa kuziharibu roho zetu..

Shalom…

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *