Elewa maana ya Mathayo 10:41 ampokeae Nabii atapata thawabu ya Nabii.

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom!, Nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo.

Ni Thawabu gani haswa ilikuwa ikizungumziwa hapo?.

Tukianza kusoma Mathayo 10:41 kwa makini na ule Mstari wa 41. Tutapata Thawabu haswa iliyokuwa inazungumziwa hapo ni ipi?.

Mathayo 10:41″Ampokeaye nabii kwa kuwa ni nabii, atapata thawabu ya nabii; naye ampokeaye mwenye haki kwa kuwa ni mwenye haki, atapata thawabu ya mwenye haki”

Sasa ukiemdelea kusoma jibu liko katika Mstari ule wa 42 hebu tusome…

Mathayo 10:42 “Na mtu awaye yote atakayemnywesha mmojawapo wa wadogo hawa ngaa kikombe cha maji ya baridi, kwa kuwa ni mwanafunzi, amin, nawaambia, HAITAMPOTEA KAMWE THAWABU YAKE”.

Thawabu inayozungumziwa hapo ni Thawabu kutoka kwa Mungu na sio kwa yule Nabii. Kivipi?, kwa jinsi tunavyowapokea/kuwakaribisha na kuwajali pale tunapokutana nao mitaani,majumbani petu,makazini, safarini nk.

Unapompokea mtu wa Mungu kwa Heshima kubwa kwa kumjali na kumsikiliza na ndivyo Mungu atakavyokuchukulia kuwa ni mtu wa heshima(atakuheshimisha) na kukubariki sana na kukujali pia kama ulivyomjali mtumishi wake.

Na pia kama ukimpokea kama mtu wa kawaida tu na kumsikiliza tu ili aondokke ndio hivyo hivyo pia Mungu atakavyokuchukulia pia.
Na kama ukimlaani vivyo hivyo na kwako itakuwa yeye hatapatwa na dhara lolote ila wewe uliefanya kitendo kile.

Kama vile Bwana wetu alivyosema

Luka 6:38 “Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, NDICHO WATU WATAKACHOWAPA VIFUANI MWENU. KWA KUWA KIPIMO KILE KILE MPIMACHO NDICHO MTAKACHOPIMIWA”.

Hivyo kipimo upimacho kwake na kwa mtu yeyote ndicho hicho hicho utakachopimiwa ndugu.

Hivyo tukishalijua hili na sisi pia hatuna budi kutia bidii katika kuwapimia watumishi wa wa Mungu na watu wengine pia vipimo vizuri maana ndio tutakavyopimiwa.

Bwana azidi kutuongezea Neema na tufanyike kuwa ni miongoni mwa watu wa kubariki n kubarikiwa na yeye Baba yetu.

Maranatha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *