Maana ya Karama ya pili 2 Wakorintho 1:15.

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom!, Nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo.

Katika Maandiko/Biblia mahali pengine unapokuta mahali Neno limeandikwa “Karama” si wakati wote maana yake inabakia kuwa vilele tu la!, maana karama kwa maana nyingine ni “Zawadi”

Ukisoma walaka wa Mtume Paulo kwa Warumi Kuna mahali anasema “….Bali Karama ya Mungu ni uzima wa milele..” Sasa je Mungu anakarama maalumu? Kama sisi jibu ni la!, Mungu hana karama maalumu maana yeye vyote vyatoka kwake!.

Warumi 6:23 “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu”.

Maana yake ni kwamba “Mapenzi ya Mungu au zawadi ya Mungu/baraka ya Mungu kwetu sisi ni uzima wa milele.”

Sasa tusome walaka wa pili kwa Wakorintho kwa makini tuone ni karama ipi alikuwa anaizungumzia Mtume Paulo.

2Wakorintho 1:15 “Nami nikiwa na tumaini hilo nalitaka kufika kwenu hapo kwanza, ili mpate karama ya pili

Vivyo hivyo pia mtume Paulo aliposema hivyo hakumaanisha karama nyingine(mpya)zaidi ya hiyo aliyokuwa nayo ya kitume la!,  kusudi kubwa hapo Paulo alimaanisha “Baraka ya pili”.

Ni sawa na mtumishi aliekwenda kufanya Semina Shinyanga, labda ya wiki moja harafu akamaliza akarudi dar es salaam nyumbani anakochunga kanisa kisha baada ya wiki mbili akapata tena Neema ya kwenda kufanya semina Mwanza.  Ni lazima atapita shinyanga wakati wa kwenda na wakati wa kurudi pia Sasa wakati anarudi dar es salaam baada ya kumaliza Semina yake mwanza akaona si vyema kuwapita watu wa shinyanga bila kuwasalimia akawasiliana nao na kuwaambia atapita hapo kuwasalimia na kufanya semina walau ya siku moja atakapopita basi watu wa shinyanga watakuwa wamepata karama ya pili yaani “Baraka/zawadi ” kwa mtumishi huyo kupita tena.

Vivyo hivyo Paulo alikuwa ameshapita watu wa Korintho kuwafundisha/kuwahubiria Neno na kuwabariki, lakini alitaka tena kupita hapo mara ya pili  wakati anaelekea kuwafundisha watu wa Makedonia. Ili wapate Baraka mara mbili.

Hivyo Paulo alikuwa akipitia changamoto nyingi sana katika kuhubili injili lakini hakutaka tamaa alikuwa ni mtu wa kujibidiisha sana. Na hata kurudi mara mbili ama mara tatu sehemu ile ile tu haijalishi alipigwa na kutaka kuuliwa Lakini alikuwa akirudi. Vivyo hivyo na sisi Mungu atujalie nguvu kama ya Mitume katika kuifanya kazi yake.

Matendo 15:36 “Baada ya siku kadha wa kadha Paulo akamwambia Barnaba, Haya! Mrejee sasa tukawaangalie hao ndugu katika kila mji tulipolihubiri neno la Bwana, wa hali gani”.

Ubarikiwe saa.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *