Nini maana ya kupatiliza?

  Maswali ya Biblia

Kupatiliza lina maana ya kupiga/kuadhibu, mfano mzuri tunaweza kusema mtu huyu amepigwa na Mungu ni sawa na kusema mtu huyu amepatilizwa na Mungu..

Jambo la kujiuliza je Mungu anapiga watu (anapatiliza)?

Jibu la uhakika ni ndio, Mungu Anatoa adhabu, anapatiliza waovu, na wema kama ikiwa watapita kinyume na njia zake..

Kusudi la Mungu kutuadhibu ni ili tutubu na kumrudia yeye si kutukomoa au kukomesha kama tufanyavyo sisi wanadamu 

Tunapopitia magumu fulani au changamoto tofauti tofauti kusudi kuu la Mungu ni ili tutubu na kuziacha njia zetu mbaya tunazoziendea na kumrudia yeye, hapo Bwana atayaondoa mapatilizo yote na kutuletea mema juu yetu..

Tumwangalie nabii Yona alipigwa na Mungu kwasababu aliliacha kusudi la Mungu akategemea atakuwa salama, kumbe ndivyo jinsi anavyozidi kuelekea katika hatari zaidi,akajikuta yumo ndani ya nyangumi siku tatu,mchana na usiku, bila kunywa wala kula..

Vivyo pia Bwana anasema awapatiliza waovu mpaka kizazi cha tatu

Kutoka 20:4-5[4]Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.

[5]Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,

Ukiwa ni  mtu wa kuabudu miungu mingine tofauti na Mungu wa Mbinguni,unaabudu mizimu,sanamu kwasababu na wazazi wako walifanya hivyo basi fahamu utapatilizwa ikiwa utaendelea na wewe kuabudu sanamu..

Mamlaka hayo pia ya kwenda kupatiliza yapo kwa wana wa Mungu,waliotakaswa kwa damu ya Yesu Kristo,tunapatiliza kazi zote za adui shetani na kuwaweka huru watu mateka…

2 Wakorintho 10:2-6
[2]naam, naomba kwamba nikiwapo, nisiwe na ujasiri kwa uthabiti ambao nahesabu kuwa nao juu ya wale wanaodhania ya kuwa sisi tunaenenda kwa jinsi ya mwili.


[3]Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili;


[4](maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)


[5]tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;


[6]tena tukiwa tayari kupatiliza maasi yote, kutii kwenu kutakapotimia.

Tunapatiliza/Kuzipiga ngome za adui shetani kwa KUOMBA NA KUSOMA NENO PAMOJA NA KUHUBIRI

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT