Mithali 30:32-33[32]Ikiwa umefanya kipumbavu kwa kujikuza; Au ikiwa umewaza mabaya; Basi weka mkono wako juu ya kinywa chako.
[33]Kwa maana kupiga maziwa huleta siagi; Na kupiga pua hutokeza damu; kadhalika kuchochea hasira hutokeza ug
omvi.
Maandiko yanatupa kuelewa kwamba kila tendo lolote linalofanyika kwa uzuri au ubaya,basi fahamu tu litaleta majibu tu.. Hapo ametumia mfano wa siagi ambao upatikanaji wake ni kwenye maziwa, na tabia yake ni kujificha ndani ya maziwa,na ili uipate siagi ni lazima uyapige maziwa ili ipande Kwa juu..
Na si kitendo cha kuyapiga maziwa tu bali kuyakoroga kwenye chombo baada ya muda,maziwa na siagi vinajitenga vyenyewe..
Hivyo hivyo kwenye upande wa pua,ndani yake damu ipo lakini mpaka ionekane imetoka nje basi imepigwa,mfano ni mtu akupige ngumi au kitu kizito kwenye pua lazima damu itatoka tu,
Ugomvi nao umefananishwa hivyo hivyo,ni jambo ambalo lipo tu katikati yetu,sawa na siagi ndani ya maziwa na damu ndani ya pua, na ugomvi ili uonekane basi lazima uchochewe na kukorogwa sana,.. Kwasababu hasira zinapoanzia Katika mazungumzo mabaya na mwenzako akakereka na Maneno hayo, biblia inasema weka mkono wako kinywani usiendelee na kuongea kwasababu kitakachofuata ni mapigano na kuumizana..
Vitu vingi kama uuaji,wivu,chuki, visasi vinatokana na hasira zilizochochewa sana..
Lakini Kumbuka uwezo huu wa kujizuia haupo kwa kila mtu ikiwa upo nje ya wokovu, mwamini Yesu Kristo moyoni mwako..
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa Mawasiliano: +255693036618,255789001312
Bwana akubariki.