NINI MAANA YA NENO KALIBU?

Maswali ya Biblia No Comments

Mathayo 6:30 “Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?”

Kalibu ni neno lililorudiwa na kutajwa Katika kitabu cha Luka 12:28,, na maana ya Neno hili ni TANURU LA MOTO…, Ni kawaida ya kila mmoja baada ya kusafisha mazingira huwa takataka tunatupa kwenye tanuru ya moto, sasa hiyo tanuru ya moto tunaweza kuiita Kalibu, ndo mana tunaona hapo Bwana Yesu ameyapa uthamani maisha yetu kuliko maua ya kondeni…

Ikiwa Mungu anayapendezesha maua ya kondeni na kuyastawisha ambayo mwisho wa siku hutupwa motoni, sisi tunauthamani sana Mbele za Mungu kuliko maua, anaweza kutuvisha kuliko hayo maua, anaweza kutulisha kuliko ndege yeyote yule na kubarikiwa zaidi.. ni Neema ya ajabu sana…

Kikubwa kwetu ni sisi kuutafuta Ufalme wake kwanza na hayo yote amesema atatuzidishia, na sikuzote Mungu hasemagi uwongo..

Luka 12:29 “Ninyi msitafute mtakavyokula wala mtakavyokunywa; wala msifanye wasiwasi,

30  kwa maana, hayo yote ndiyo watafutayo mataifa ya duniani, lakini Baba yenu anajua ya kuwa mna haja na hayo.

31  Bali utafuteni ufalme wa Mungu, na hayo mtaongezewa.

32  Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule ufalme”

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Mafundisho zaidi, NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *