DINI NI NINI?

Maswali ya Biblia No Comments

Jibu..

Dini ni kitendo cha kuamini imani fulani hasa mambo ya rohoni, Mtu anapoamini uwepo wa Mungu au vitu vyovyote visivyoonekana na kuanza kuviabudu kwa kuvifanyia ibada basi hapo ulazima wa dini kuumbika ni lazima….

ndipo hapo utaona utaratibu fulani au ustaarabu unaanza kutengenezwa na kufatwa, tukiangalia wanaoifata imani ya Buddha, wamejiwekea taratibu zao za kufatwa ili kumwabudu mungu wao ipasavyo, ndipo hapo utaona wamejiwekea sheria ya mavazi fulani, maisha ya kujinyima na kutoshirikiana na jamii, au kutokula baadhi vya vyakula…n.k, Sasa hiyo ndiyo inaitwa dini..

Hayo pia tunayaona kwa Yule mtu aliyemwamini YESU KRISTO kweli kweli, kuna kiwango cha dini kinakuwa ndani yake, Mkristo huyu utaona anaanza kuwa mtu wa kupenda kuomba sana, anajijengea utaratibu yeye mwenyewe wa kuanza kusoma biblia na kwenda kuwashuhudia na wengine habari za Yesu Kristo, haachi kwenda kanisani kwa kila ibada, anajiwekea utaratibu wa kumtolea Mungu sadaka na kuwasaidia na wengine na zaidi ya hayo… Ndo mana Maaandiko yanasema….

Yakobo 1:26 “Mtu akidhani ya kuwa anayo dini, wala hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hali akijidanganya moyo wake, dini yake mtu huyo haifai.

27 Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.”

Hivyo dini ya kweli ni hiyo tunayoisoma kwenye mstari wa 27 ingawaje haitupi uhalali wa Moja kwa moja wa kwenda Mbinguni bali inatupa njia na kuturahishia kwenda Mbinguni, ijapokuwa wengine wanaamini ukiwa mtu wa dini ndio umeokoka, Katika Ukristo USIPOMWAMINI YESU KRISTO, ukamkiri kwa kinywa chako na kubatizwa ubatizo sahihi, hata uwe mtu wa dini kiasi gani, wewe Mbinguni utapasikia tu,huwezi kwenda…

Kuna watu wanajibidiisha sana Katika dini zao, ni mtu wa kufunga sana, lakini ikiwa Maisha yako yako mbali na Yesu Kristo fahamu tu kuzimu inakungoja, dini si kitu cha kujivuna, kwasababu tiketi ya sisi kumuona Mungu na kumkaribia ni Roho Mtakatifu, kama hauna huyo basi kwako ni sawa na bure…

Kwasababu dini iliyo Katika kweli itaambatana na Imani ipasavyo.. Imani ya kweli ni ile iliyopo katika kumwamini Yesu Kristo kama mwana wa Mungu na aliyetumwa kuja kuwaokoa wanadamu. Hiyo ndiyo imani ya kweli..Imani nyingine tofauti na hiyo ni imani ya uongo na inayopotosha na kupeleka watu mautini.

Tukishayafahamu hayo hatuna budi kujivunia wokovu mkuu Katika Yesu Kristo, Kwa upendo wake mwingi alioutoa kwa ajili ya maisha yetu, Ikiwa bado hujaingia ndani ya imani hii ya Yesu Kristo bado ujachelewa, mlango wa Neema umefunguliwa juu yako, mgeukie Kristo leo kwa kutubu dhambi zako zote na kuoshwa kwa damu yake, naye atakusamehe na kukurehemu.

Shalom…

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Mafundisho zaidi, NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *