NENO SAUMU LINA MAANA GANI KATIKA BIBLIA ?

  Maswali ya Biblia

Jina la Mwokozi wetu litukuzwe, nakukaribisha katika kujifunza Neno la Mungu litupalo uzima wa milele…

Je saumu ina maanisha nini katika Biblia ?
Saumu ni neno la kiaramu lenye maana ya KUJIZUIA, kujizuia kufanya jambo/kitu Fulani kwa ajili ya ibada, au kwa maana nyingine saumu inamaanisha mfungo.
ndipo hapo utakuta mtu anaacha kula kwa kipindi Fulani, ili kukutumia kipindi hicho kufanya sala na kumtafakari Mungu. katika kipindi hiki tunaweza sema mtu huyo yupo katika mfungo

Neno hilo utalipata katika vifungu hivi kwenye biblia..
Zekaria 8:19
[19]BWANA wa majeshi asema hivi, SAUMU ya mwezi wa nne, na saumu ya mwezi wa tano, na saumu ya mwezi wa saba, na saumu ya mwezi wa kumi, zitakuwa furaha na shangwe, na sikukuu za kuchangamkia, kwa nyumba ya Yuda; basi zipendeni kweli na amani.

Yoeli 1:14
[14]Takaseni SAUMU, iteni kusanyiko la dini,
Wazee na wakusanye wenyeji wote wa nchi; Waende nyumbani kwa BWANA, Mungu wenu, Na kumlilia BWANA,

Soma pia Yoeli 2:15.utaliona neno hilo.

NI SAUMU IPI AMBAYO TUNATAKIWA KUFANYA

Japo kuwa imezoeleaka na wengi kuwa saumu au mfungo ni ule tu wa kujizuia kula chakula basi, ni kweli lakini lipo kusudi ambalo Mungu alilikusudia mahali hapa katika saumu zetu
tusome
Isaya 58:3-8
[3]Husema, Mbona tumefunga, lakini huoni? Mbona tumejitaabisha nafsi zetu, lakini huangalii? Fahamuni, siku ya kufunga kwenu mnatafuta anasa zenu wenyewe, na kuwalemea wote watendao kazi kwenu.

[4]Tazama, ninyi mwafunga mpate kushindana na kugombana, na kupiga kwa ngumi ya uovu. Hamfungi siku hii ya leo hata kuisikizisha sauti yenu juu.

[5]Je! Kufunga namna hii ni SAUMU niliyoichagua mimi? Je! Ni siku ya mtu kujitaabisha nafsi yake? Ni kuinama kichwa kama unyasi, na kutanda nguo za magunia na majivu chini yake? Je! Utasema ni siku ya kufunga, na ya kukubaliwa na BWANA?

[6]Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira?

[7]Je! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe?

[8]Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia; utukufu wa BWANA utakufuata nyuma ukulinde.

Umeona hapo Kumbe, kusudi la Mungu kuruhu saumu au mifungo, halikuwa tu Kwa kujinyima chakula au kuutabisha nafsi kumbe, lengo kuu zaidi lilikuwa ni kufungua vifungo vya uovu,.
hivyo katika kufunga kwako hakikisha unapambana kukamilisha tabia au mienendo yako iwe katika kumpendeza Mungu ili funga yako isiwe bure tu, kwa kuwa na chuki na jirani yako, kinyongo na mpendwa wenzako,hasira, wivu, nk mambo kama haya unapaswa kushughulika nayo, Na isiwe Kwa kipindi tu, Bali inapaswa baada ya kuomba basi uanze kuyaishi siku zote za maisha yako
hiyo ndiyo saumu Mungu aliyoichagua, sisi kuacha na vifungo na nira.

Bwana akubariki

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT