Nini maana ya kuungama?

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom!,

Kuungama ni kukiri/kukubali hadharani katika mkusanyiko wa waamini au baina ya watu wawili, mfano pale mtu anapoamua kuzikiri dhambi zake kwa Imani kwa kumuamini Yesu Kristo awe Bwana na mwokozi wa maisha yake, Kwa kudhamiria kabisa kuacha dhambi na kuamini huyo anakuwa tayari amepata msamaha wa dhambi na uzima wa milele, Sasa jambo hilo tunaweza kusema huyo mtu ameungama/amekiri.

Mathayo 3:5 Ndipo walipomwendea Yerusalemu, na Uyahudi wote, na nchi zote za kandokando ya Yordani;

6 naye akawabatiza katika mto wa Yordani, huku wakiziungama dhambi zao”.

1Yohana 1:9 “Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote”.

Hivyo mtu anapokiri dhambi zake mbele ya watu akitaka kuokoka huyo ameweka wazi maana yake ameungama. Hata pale tunapoikiri Imani yetu kuwa sisi tu wa Kristo Yesu na Bwana wetu alikufa na kufufuka hiyo tunakiri kuwa sisi ni Wakristo kweli kweli.

Kama vile Bwana wetu Yesu Kristo alivyokiri mbele ya Pontio Pilato alipomuuliza kuwa wewe ndiwe Kristo Bwana wetu alikiri kwa kusema “WEWE WASEMA” yaani manaa yake ni “KAMA ULIVYOSEMA”

Ukisoka Amplified Bible inasema.

Luke 23:3 “So Pilate asked Him, Are You the King of the Jews? And He answered him, [It is just as] you say. [I AM.]”

Unaona hapo! “IT IS JUST AS YOU SAY” Maana yake ni ile ile “KAMA ULIVYOSEMA”

“I AM” yaani “Ndio Mimi”. Hivyo Bwana wetu Yesu alikiri wala hakuficha kuwa yeye ndie Kristo.

Pia alipopelekwa kwa wakuu wa makuhani na waandishi utaona alipoulizwa na Kuhani Mkuu Kayafa vivyo hivyo pia alikiri kuwa yeye ndiye.

Hivyo kila mahali ambapo Bwana Yesu aliulizwa kama yeye ndie Masihi yaani alikiri.

Hivyo hata sisi pia inatupasa kuikiri Imani yetu. Mahali popote pale tunapoingia na kutoka Imani yetu juu ya Bwana wetu Kristo Yesu yeye alie muanzilishi wa Imani yetu wala tusifiche kabisa kwa kuwaogopa watu fulani fulani bali tukubali kuwa ndio tumemwamini Kristo na tulikuwa pamoja nae na kukufuka pamoja nae kwa njia ya Ubatizo kama maandiko yanavyosema na tu warithi pamoja na Kristo Yesu HALELUYA!!.

1Timotheo 6:12 “Piga vita vile vizuri vya imani; shika uzima ule wa milele ulioitiwa, UKAUNGAMA MAUNGAMO MAZURI MBELE YA MASHAHIDI WENGI”.

Hivyo kama maandiko yanavyosema kuwa tuyashike sana, sio kidogo bali sana Maungamo yetu.

Waebrania 4:14  “Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *