JE SHETANI NI NANI?

Maswali ya Biblia No Comments

Maana halisi ya jina shetani ni Mshitaki” au kwa lugha nyingine Mchongezi, na kazi yake kubwa ni kuwashitaki watakatifu mbele za Mungu.. hiyo ni moja ya kazi yake kubwa anayoifanya shetani..

Maana nyingine ya jina shetani ni LUSIFA, ikimaanisha NYOTA YA ASUBUHI” (Isaya 14:12) hili lilikuwa jina lake kabla ajaasi, alivyoasi Mbinguni akawa shetani….

Kabla ajamwasi Mungu, shetani alikuwa ni malaika wa sifa(Kerubi), alikuwa na ukamilifu wote Katika njia zote, ikampelekea kupata kibali na kukubaliwa na Mungu kuliko malaika wengine (Ezekieli 28:14).. aliendelea na ukamilifu wake mpka siku uovu wake ulipoonekana ndani yake (Ezekieli 28:15)…

Kwasababu ya kupata uzuri , moyo wake ukaanza kuinuka na kuanza kujiona anaweza kuwa kama Mungu na ndo hapo akaanza kuwashawishi 1/3 ya malaika ili washikamane naye…

Biblia inasema kulitokea vita vikali kati ya malaika walioasi na wale waliokataa kuungana na lusifa, ijapokuwa haijaeleza kwa undani vita hivyo lakini Mwisho wa siku tunaona lusifa na malaika zake wakashindwa na kutupwa chini duniani Ufunuo 12:7).

Lakini bado tunaona vita bado vinaendelea ijapokuwa vita vya kwanza vilipiganwa Mbinguni, na walio upande wa Mungu wakashinda, ila vita vya pili bado vinaendelea ndani ya ulimwengu huu na Mwisho wake ni ile siku ya mwisho, yaani mwisho wa dunia..

Shalom,

Mpokee Yesu Kristo Maishani mwako ili akupe nguvu za kushinda vita vya shetani, Uwezo una yeye Mungu wetu…

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Mafundisho zaidi, NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8j

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *