FADHILI NI NINI?

Maswali ya Biblia No Comments

Maandiko yanapozungumzia kuhusiana na fadhili za Mungu basi tufahamu ni zaidi ya zile fadhili ambazo tunaweza kuzifanya kwa kuonyeshana ukarimu na wema…

Ndani ya biblia fadhili za Mungu ni neno pana sana na hatuwezi kusema tunalielezea kwa neno moja ili tupate maana kamili hata kwa Maneno machache,…Kwa lugha ya Kiebrania linaitwa Hesed”..

Fadhili za Mungu sio Mambo tu tunayoyaona ambayo kibinadamu tunaweza kuyafanya bali ni ule Upendo wa KiMungu usioweza kuelezeka , Yani huwezi kuuelezea, ni upendo wa kusaidia , unavumilia, ni Upendo wa kutoa na kuokoa pasipo na sababu,

Ni mambo makubwa sana anayotutendea Mungu pasipo kujali kwamba tulimtendea kitu gani kwanza, ni kama wajibu wake kututendea,ni wema ambao hauwezi kuelezeka, unagusa kila nyanja ambazo haziwezi kufikiwa na mwanadamu yeyote , kiumbe cha mbinguni au duniani, ni wema ulioingia ndani sana..

Neno hili pia tunaweza kulipata sehemu mbalimbali Katika Maaandiko, na wakati mwingine Daudi alichokiona alihitimisha na neno, “Kwa maana fadhili zake ni za milele”

Zaburi 136:1-4,6-16
[1]Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.


[2]Mshukuruni Mungu wa miungu;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.


[3]Mshukuruni Bwana wa mabwana;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.


[4]Yeye peke yake afanya maajabu makuu;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.


[6]Yeye aliyeitandaza nchi juu ya maji;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.


[7]Yeye aliyefanya mianga mikubwa;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.


[8]Jua litawale mchana;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.


[9]Mwezi na nyota zitawale usiku;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.


[10]Yeye aliyewapiga Wamisri kwa kuwaua wazaliwa wa kwanza wao;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.


[11]Akawatoa Waisraeli katikati yao;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.


[12]Kwa mkono hodari na mkono ulionyoshwa;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.


[13]Yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.


[14]Akawavusha Israeli katikati yake;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.


[15]Akamwangusha Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.


[16]Yeye aliyewaongoza watu wake jangwani;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Jambo hili tunaliona pia kwa Musa , Mungu alipomfumbua macho yake ili amwelewe kwa sehemu, Musa alitangaza kwa kusema..

Kutoka 34:6 “Bwana akapita mbele yake, akatangaza, Bwana, Bwana, Mungu mwingi wa huruma, MWENYE FADHILI, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli;

Ndo hicho kilichomfanya Mungu kumtoa na kumtuma Mwanae wa pekee kwa ajili ya kuuokoa ulimwengu, hakukuwa na sababu yeyote zaidi tu ya FADHILI ZAKE ZA MILELE ZINZODUMU KWETU DAIMA,ukilijua hilo utampenda Mungu na Kumshukuru sana…

Tukiyafahamu hayo hatuna budi Kumtukuza, Kumsifu na kumshangilia Mungu wetu kwa fadhili zake za kumtoa Mwanae mpendwa, jambo ambalo hata wewe mwenyewe huwezi kulitenda,umtoe mwanao unayempenda kwa ajili ya jirani yako ambaye hana msaada wowote… Huwezi kufanya hivyo kwasababu hujafikia kiwango hicho cha fadhili za Mungu..Embu anza sasa Kumshukuru Mungu kwa wema wake aliotuonyesha pamoja na Matoleo yetu kwa Mungu..

Sifa, Heshima na utukufu ni vyako Mungu wetu…

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *