NENO SHEHE LINA MAANA GANI?

Maswali ya Biblia No Comments

Neno Shehe limetokana na asili ya lugha ya kiarabu. Kama ambavyo tunafahamu asili ya lugha ya Kiswahili inatokana na kutoholewa kwa maneno ambayo asili yake ni kiarabu mfano wa maneno hayo ni salamu,sultani,sadaka,shukrani adhabu,adui,jehamu,dhamira damu,giza lawama,askari,roho,tufani,simba,msalaba,sheria,raisi,sultani,na uashratink.k hivyo theluthi ya lugha ya kiswahili ni kiarabu.

Kwa kuwa waarabu waliishi hapo zamani katika nchi yetu na kwa wakati huo lugha yetu ilikuwa haijajitosheleza ikapelekea sisi kutumia maneno yao katika lugha yetu.Na sio waarabu pekee bali pia na watawala wengine enzi za ukoloni waliotutawala nchini.

Hivyo kwa kuwa waarabu walikuwa wanatawala katika nchi yetu huko zamani zile na lugha yetu kwa kiasi fulani ilikuwa bado haijajitosheleza hivyo tukajikuta tunalazimika kutumia maneno yao katika lugha yetu, na sio kiharabu tu hata na lugha nyingine za kigeni za watu waliotawala nchi yetu…

Kwa hiyo neno SHEHE kwa asili yake ni kiharabu, likiwa na linmaanisha Kiongozi, au mwalimu hususani anayehusiana na mambo ya kidini..na ndio maana ukisoma katika tafsiri nyingine za kibiblia mfano za biblia za kiingereza utakuta neno Lords, or rulers ndio linatumika …
Neno Shehe unaweza ukaliona katika kitabu cha Yoshua 13:3,21, 17:7, 1Samweli 5:7,11, 6:4, Ezra 9:2 Nehemia 2:16

Kwakuwa neno Shehe linatumika sana na waumini wa kiislamu linatambukika na kujulikana kama ni la kiislamu lakini kwa asili yake ni neno la kiarabu.Neno Shehe linatumika sana katika jamii ya waarabu haswa waislamu likiwa na maana ya viongozi wa dini ya kiislamu na ndio maana linaonekana kama ni neno la kiislamu lakini kiuhalisia sivyo..

Halkadhalika pia Neno Rabi kama ni neno linalomaanisha mwalimu kwa kiyahudi, lakini kwasababu ni neno ambalo limetokana na lugha ya kiyahudi na linatumika sana na viongozi wa dini ya kiyahudi basi linajulikana hivyo kuwa mtu awaeyeyote anayejiita Rabi yeye ni kiongozi wa dini ya kiyahudi lakini kiuhalisiasio hivyo hata kiongozi wa dini nyingine tofauti na ya kiyahudi anaweza kuitwa Rabi kwasababu maana halisi ya neno Rabi ni mwalimu…

Vile vile neno Mchungaji hutumika na viongozi wa dini ya kikristo, na huwa halitumiwi mara nyingi na viongozi wa dini nyingine lakini kiuhalisia hata hao viongozi wa dini nyingine wanaweza kuitwa mchungaji . Na ndivyo ilivyo hata kwa Neno shehe, pamoja na mengine tuliyo yaona .

Pia kutika agano jipya neno shehe halijatumika Sana badala yake maneno kama mchungaji na mwalimu ndio yametumika Lakini kwa Lugha ya kiharabu linamaanisha watu hao hao

Ubarikiwe sana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *