Nyamafu ni nini?

Maswali ya Biblia No Comments

Nyamafu ni mnyama aliekufa bila kuchinjwa au aliekufa kwa kularuliwa na mnyama mwingine(kama simba kumlarua nyati.) Yaani kitu chochote Chenye uhai kilichokufa kibudu bila kuchinjwa.

Katika Agano la Kale Mungu aliwakataza wana wa Israeli kula nyamafu, yaani wasile mnyama wana aina yoyote aliekufa bila kuchinjwa maana wakifanya hivyo watajitia unajisi mbele za Mungu.

Walawi 17: 15 “Tena kila mtu atakayekula NYAMAFU, au nyama aliyeraruliwa na wanyama, kama ni mzalia, kama ni mgeni, atafua nguo zake, na kuoga majini, nayeatakuwa najisi hata jioni; ndipo atakapokuwa safi.

16 Lakini kwamba hazifui, wala haogi mwili, ndipo atakapochukua uovu wake”.

Ukisoma tena

Mambo ya Walawi 22:8 “Nyamafu au mnyama aliyeraruliwa na wanyama asile, asijitie unajisi kwa hiyo nyama; mimi ndimi BWANA.”

Mungu aliwakataza wasile nyamafu maana ni nyama ambayo ilikuwa na damu ndani yake. Kwa namna gani?

Je Kuna nyama isiyokuwa na damu?, Kuna utofauti upo kati ya mnyama aliyekufa na aliyechinjwa kiwango cha damu kinatofaitiana!, aliekufa na mwenye damu inakuwa ni nyingi zaidi ndani yake tofauti na aliechinjwa.

Ni agizo ambalo Mungu alilitoa katika kile kitabu cha Mwanzo sura ya 9.

Mwanzo 9: 3 “Kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyowapa mboga za majani, kadhalika nawapeni hivi vyote. 4 Bali nyama pamoja na uhai, yaani, damu yake, msile”

Maana uhai wa mnyama au mtu uko katika damu.

Ukisoma pia

Ezekieli 33:25 “Basi, waambie, Bwana MUNGU asema hivi; MNAKULA NYAMA PAMOJA NA DAMU YAKE, na kuviinulia vinyago vyenu macho yenu, na kumwaga damu; je, mtaimiliki nchi hii”

Utaona wana wa Israeli waliyaasi maagizo ya Bwana wakaanza kula nyama pamoja na damu yake.

Je!, ni sahihi kwa sasahivi kula nyamafu.

Kimsingi na kwa sababu za kiafya pia si sawa kula nyamafu yaani mnyama aliekufa

mwenyewe maana hujui kafa kwa sababu gani?, pia kwa hali ya kawaida tu ni lazima dhamiri yako itakuwa inakinzana na wewe kula mnyama aliekufa mwenyewe ijapokuwa ukilazimisha unaweza kula japo dhamiri yako inakinzana na wewe.

Je!, kitu gani katika roho kinafunua katika kumchinja mnyama(ilikuwa inawakilisha nini katika roho)?.

Hii ilikuwa ikimfunua Bwana wetu Yesu Kristo ili aweze kuleta ukombozi kwetu sisi ilimbidi afe na damu yake imwagike pale msalabani ndipo ilete uhai kwetu sisi ambao tulikuwa tumekufa kwa sababu ya dhambi zetu. Hivyo kama Kristo angeliishi mpaka akafa kama Yohana damu yake isingelimwagika na tusingepata ukombozi.

Hivyo ukombozi wetu sisi tumeupata kwa Bwana wetu kuchinjwa pale msalabani.

Hivyo chakula halisi cha ulimwengu huu ni Kristo Yesu maana alichinjwa na hakuwa nyamafu.

Yohana 6:31 “Baba zetu waliila mana jangwani kama vile ilivyoandikwa, Aliwapa chakula cha mbinguni ili wale.

32 Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Siye Musa aliyewapa chakula kile cha mbinguni, bali Baba yangu anawapa ninyi chakula cha kweli kitokacho mbinguni

33 Kwa maana chakula cha Mungu ni kile kishukacho kutoka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima.

34 Basi wakamwambia, Bwana, sikuzote utupe chakula hiki.

35 Yesu akawaambia, Mimi ndimi chakula cha uzima; yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe.”

Usitumainie nyamafu yaani ulimwengu huu na mambo yake maana hautakupa uhai wa roho yako bali mtunainie Kristo Yesu yeye ndio kweli na uzima.

Mambo yote unayohangaikia hayatakupa uzima wa milele yote ni nyamafu pasipo Kristo Yesu.

Ubarikiwe na Bwana Yesu.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo

Pia unaweza kujiunga na channel yetu ya mfundisho ya NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *