NYUNI NINI?

Maswali ya Biblia No Comments

Je nyuni ni nini kama tusomavyo katika maandiko

Nyuni ni neno linalomaanisha ndege.

Baadhi ya vifungu katika biblia vinavyolitaja neno hilo;

Mathayo 13:31 “Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na punje ya haradali, aliyoitwaa mtu akaipanda katika shamba lake;

32 nayo ni ndogo kuliko mbegu zote; lakini ikiisha kumea, huwa kubwa kuliko mboga zote, ikawa mti, hata nyuni wa angani huja na kukaa katika matawi yake”.

Zaburi 102:5 “Kwa ajili ya sauti ya kuugua kwangu Mifupa yangu imegandamana na nyama yangu.

6 Nimekuwa kama mwari nyuni wa jangwani, Na kufanana na bundi wa mahameni”.

Sefania 2:14 “Na makundi ya wanyama watalala kati yake, wanyama wote wa mataifa; mwari-nyuni na nungu watakaa juu ya vichwa vya nguzo zake; sauti yao itasikiwa madirishani; vizingitini mwake mtakuwa ukiwa; kwa maana ameifunua kazi ya mierezi”.

Soma pia Kumb 14:11,Ayubu 12:7

Katika biblia watu wa mataifa (wasiomcha Mungu) wanafananishwa na nyuni wa angani, na ndio maana utaona Bwana Yesu anaufananisha ufalme wa mbinguni na chembe ya haradani na kusema japo ni ndogo kuliko mbegu zote..Lakini inapokuwa ndani ya mtu inabadilika na kukua kwa ukubwa, kiasi cha kutoa matawi makubwa na watu kuketi chini yake na kupumzika (yaani kujifunza Neno la Mungu, na kupokea baraka zote)

Hivyo nasi pia tunapewa hamasa, tuwe na bidii ya kupenda kuutafuta ufalme wa Mungu, kwani kwa wakati wasasa tulionao waweza kuonekana ni kitukisichokuwa na manufaa lakini kama tukiendelea kuweka bidii na kumaanisha kumtafuta Mungu na kutaka kujua mapenzi yake ni yapi katika maishani yetu. Ndivyo Basi kwa wakati ujao tutaweza kuwa ni msaada mkubwa kwa maelfu ya watu(Nyuni) kumjua yeye.

Bwana akubariki.

Kwa Maswali/ Maoni/Maombezi au Ratiba za Ibada wasiliana nasi Kwa namba
+225693036618/ +225789001312

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *