NENO MBARI LINA MAANA GANI?

Maswali ya Biblia No Comments

Jina la Bwana wetu Yesu litukuzwe karibu katika kujifunza maneno ya uzima ya Bwana wetu Yesu kristo .


Katika biblia takatifu yapo maneno ambayo tunakutana nayo wakati tunasoma maandiko na tunakuwa hatufahamu maana ya maneno hayo
Tutaangalia moja ya neno nalo ni MBARI.

Je neno mbari linamaanisha nini ?

Mara nyingi Neno hili linatajwa katika biblia, sana sana mahali ambapo vinatajwa vizazi vya wana wa Israeli.

Mbari, kwa namna nyingine linamaanisha neno UKOO.
Kwa Mfano unaweza kukutana na sentensi fulani inasema, “hawa ndio wakuu wa mbari za baba zao”. Hapo inamaanisha kuwa “hao ndio wakuu wa ukoo wa baba zao”,

Vifuatavyo ni baadhi ya vifungu ambavyo utakutana na Neno hilo;

1Wafalme 8:1 “Ndipo Sulemani alipowakusanya wazee wa Israeli, na wakuu wote wa kabila, wakuu wa mbari za mababa wa wana wa Israeli, wamwendee mfalme Sulemani huko Yerusalemu, ili walipandishe sanduku la agano la Bwana kutoka mji wa Daudi, yaani, Sayuni”.

1Nyakati 7:4 “Na pamoja nao, katika vizazi vyao, sawasawa na mbari za baba zao, walikuwapo vikosi vya jeshi la vita, watu thelathini na sita elfu; kwa kuwa wake zao na watoto wao walikuwa wengi”.


1Nyakati 8:28 “Hao ndio waliokuwa wakuu wa mbari za baba zao, katika vizazi vyao vyote, watu maarufu; na hao walikuwa wakikaa Yerusalemu”.


1Nyakati 9:33 “Tena hawa ndio waimbaji, wakuu wa mbari za baba zao katika Walawi, ambao walikaa vyumbani, kisha walikuwa hawana kazi nyingine; kwa kuwa walitumika katika kazi yao mchana na usiku”.


1Nyakati 26:13 “Nao wakatupiwa kura kwa ajili ya kila lango, wadogo sawasawa na wakubwa, kwa kadiri ya mbari za baba zao”.


Luka 1:26 “Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti,


27 kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, WA MBARI YA DAUDI; na jina lake bikira huyo ni Mariamu”.
Soma pia Nehemia 10:34, 11:13


Shalom.

NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *