SIKUJA KULETA AMANI DUNIANI, BALI MAFARAKANO

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom watumishi wa Mungu. Karibu tujifunze Maandiko

Kwanini bwana yesu alisema maneno haya “Sikuja kuleta AMANI duniani bali mafarakano”

Tusome

Luka 12::51 “Je! Mwadhani ya kwamba nimekuja kuleta amani duniani? Nawaambia, La, sivyo bali mafarakano

52Kwa kuwa tokea Sasa katika nyumba moja watakuwamo watu watano wamefarakana, watatu kwa wawili, wawili kwa watatu.

53Watafarakana baba na mwanawe, na mwana na babaye, Mama na binti yake, na binti na mamaye; Mkwe mtu na mkwewe, mkwe na mkwe mtu.”

Lakini tukilinganisha na mstari huu katika kitabu YOHANA

Yohana 14:27. “Amani nawaachieni; Amani yangu nawapa; niwapavyo Mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, Wala msiwe na woga”.

SWALI :

JE? Maneno haya ya bwana yesu yanakinzana yenyewe? Kama tunavyoona sehemu nyingine akiwaambia Sikuja kuleta AMANI duniani bali mafarakano.

Na nyingine “akisema Amani yangu nawaachieni”.

Mpendwa Unaposoma Maandiko hakikisha unaomba msaada wa Roho mtakatifu kukuongoza ili (kukupa mafunuo) Maana hiyo ndiyo kazi yake ( Msaidizi), La sivyo utaambulia kuona biblia ina mapungufu mengi.

JIBU :

Pale mtu anapoamua kumkabidhi Kristo maisha yake na kuachana kabisa na dhambi Kuna Mambo makuu mawili yanamtokea katika maisha yake

  1.  Kwanza kabisa anapata Amani ya moyo kwa kiasi kisichoelezeka. Yaani kuna wepesi unaachiliwa katika moyo wake mfano kama alikuwa ana hofu au kukosa matumaini basi anapata tumaini na ujasiri usio KIFANI
  2. Pia, Anapoteza Amani ya NJE!. Yaani Anapoteza Amani na ndugu jamaa na marafiki hususani wale aliokuwa akishirikiana nao katika DHAMBI! Mfano Muasherati dhidi ya Waasherati wenzake, mlevi na walevi wenzake na hata yule aliyekuwa mwenye mdomo wa masengenyo huanza kusengenywa na wale wasengenyaji wenzake hivyo kukosa amani

Ama pia wengine wanatengwa na wazazi wao, wenza wao kudhihakiwa na jamaa zao na hivyo kupoteza kabisa Ile Amani yake ya nje.

Naam, Ndipo bwana yesu anaposema alikuja kuleta mafarakano. Lakini bila kuathiri Ile Amani ya moyo au Amani ya NDANI.

GHARAMA YA KUWA MWANAFUNZI!

Yesu kristo anasema tukiamua kumfuata yeye basi hatuna budi kujitwika msalaba yaani mahangaiko au mafarakano

(Soma mathayo 10:8) Yaani ulikuwa mwizi ufarakane na wezi wenzio vivo hivyo kwa wachawi, wazinzi, wasengenyaji, Walevi n.k

Hiyo ndiyo Maana ya Bwana wetu kristo katika mstari huu (Luka 12::51)

Kwamba Sikuja duniani kuleta AMANI duniani bali mafarakano

Tuombe Mungu atusaidie na kutupa nguvu ya kulipa au kutokwepa gharama hizo za wokovu au Uanafunzi. Bali tukapate kushinda na zaidi ya kushinda. (Warumi 8:37)

Ubarikiwe

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *