Famamu maana ya 1 Wakorintho 2:12 lakini sisi hatukuipokea roho ya Dunia.

  Maswali ya Biblia

Shalom!, Nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo.

Katika ulimwengu huu tunaoishi wanadamu Kuna falme kuu mbili, yaani Ufalme wa Nuru na ufalme wa giza. Na ufalme wa Nuru ndio Roho ya Mungu. na ufalme wa giza ni roho ya ibilisi yaani roho ya Dunia.

Sasa hakuna mwanadamu ambae yupo katikati kwamba yeye hayuko katika nuru wala hayupo katika nuru. Hakuna mwanadamu awezae kujiongoza mwenyewe hapa duniani kwa roho yake. Hayupo.

1 Wakorintho 2:10-12

[10]Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu.

[11]Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu.

[12]LAKINI SISI HATUKUIPOKEA ROHO YA DUNIA, BALI ROHO ATOKAYE KWA MUNGU,makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu.

Sasa Roho ya Mungu ndio inayotufunulia yaani kuyafumbua hata mafumbo ya Mungu. Yeye ndie anaetufunulia siri za ufalme wa Mbinguni ili tuzifahamu maana hakuna mwanadamu yoyote awezae kuzijua siri za ufalme wa Mbinguni pasipo kufunuliwa na huyo Roho wa Mungu. Hekima na maarifa vyote vinatoka kwake Haleluya!.

Tunalidhibitisha hilo tukisoma…

Yohana 16:13.

[13]Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.

Hivyo mtu aliemmwamini Yesu Kristo na akapokea Roho Mtakatifu akaruhusu utendaji kazi wa Roho Mtakatifu ndani yake kamwe huyo mtu hawezi akaishi maisha ya kidunia maana Roho iliyoko ndani yake ni Roho takatifu kutoka mbinguni inayomfanya maisha ya kimbinguni wala sio ya kidunia.

Sasa kinyume chake mtu asiyekuwa na Roho wa Mungu ndani yake yaani ambae hajampokea Yesu Kristo kwanza kabisa hawezi kuishi maisha ya kimbinguni maana roho iliyo ndani yake si ya kutoka juu mbinguni bali duniani.

Nayo inafanya kazi vile vile kama ile itokayo juu!, yenyewe inawafundisha watu na kuwafunulia namna ya kuishi maisha ya kidunia hapa qmbayo mwisho wake ni uharibifu wa nafsi zo.

Ndio hapo utaona wanawake wanavaa suruali zinawabana na kuonyesha maungo yao zinawafunulia hata wanazichana mpaka mapajani ili ngozi ionekane,wanapaka make-ups na malipstick,kujichumbua ngozi,kuvaa mawigi na mahereni,ma cheni shingoni nk. Unaona vijana wananyoa viduku,kuvaa milegezo,kujichora tatoo,kwenda disco,kuzini na kufanya mapenzi ya jinsia moja na kinyume na maumbile nk ukiona hayo wewe dada, wewe kaka,mama,baba jua roho ya kidunia imekuvaa ndio maana inahuhimiza na kukusisitiza uwe wa kidunia ili uonekane unaenda na fashion na unapendeza ukiwa hivyo kumbe mwisho wa siku unakwenda kuangamia milele tubu Sasa.

Na muasisi mkubwa mwenyewe hiyo roho ni yule joka wa zamani audanganyaye ulimwengu yaani Shetani. Na kama unyakuo ukiwa ni Leo basi jua kabisa utabaki hapa hapa Duniani hutaenda na Yesu na ndio utalia na kusaga meno! Wala hutakuwa na tumaini tena geuka Sasa ni wakati wa kuuacha ulimwengu Jitwike msalaba wako umfate Yesu.

Mandiko yanatwambia….

1 Yohana 2:15

[15]Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.

Mpokee Yesu Kristo Leo itakuwa heri kwako ndugu yangu. Dunia hii haitakufikisha popote utaenda kuzimu Milele unasubili nini? Mapokee Yesu Leo upate zawadi ya bure kabisa bila gharama yoyote ya kumpokea Roho Mtakatifu atakaekuongoza na kukusaidia kuishi maisha ya kimbinguni na mwisho hata Yesu akirudi basi uwe na uhakika na ujasiri kwamba utakwenda mbinguni maana maandiko yanasema wazi wazi usipokuwa na Roho wa Mungu wewe si wake maana yake wewe ni wa ibilisi na utaenda pamoja naye.

[9]Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. LAKINI MTU AWAYE YOTE ASIPOKUWA NA ROHO WA KRISTO, HUYO SI WAKE.

Basi yathamini maisha yako Leo ndugu yangu kwa kumwamini Yesu ndio itakuwa ni salama yako. Yesu yupo njiani kurudi na maisha haya hatuishi milele je!, ukifa utakwenda wapi?.
Tengeneza njia zako Sasa kwa kumuamini Yesu Kristo.

Ubarikiwe sana.

Maranatha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT