fahamu maana ya neno shokoa katika biblia

Maswali ya Biblia No Comments

Ikiwa unasoma biblia mara kwa mara utakuwa umekutana na neno hili katika vitabu kadhaa.


Shokoa maana yake vibarua, yaani watu waliotekwa na kulazimishwa kufanya kazi kwa nguvu. Mfalme Sulemani aliwachukua watu Shokoa 2Nyakati 2:7-8
Vifungu vingine vinavyozungumzia juu ya shokoa ni 1Wafalme 5:13, Yoshua 17:13, Waamuzi 1:28, Waamuzi 1:30

Hivi leo shetani anawachukua watu shokoa, anawateka na kuwaweka chini yake wamtumikie kwa dhambi. Shetani amewanyima raha, amani wala hawana furaha wanaishi kwa hofu na wengine wamekata tamaa kwa sababu amewateka na kuwatumikisha kwa nguvu zake.

Habari njema ni kwamba yupo Yesu ambae ametiwa mafuta na Mungu ili kutusaidia tutoke katika mateka ya shetani. Yesu amekuja kutuweka huru tisiwe tena shokoa kwa adui shetani, yeye akikuweka huru unakuwa huru kweli kweli anauondoa utumwa ambao adui aliuweka. Yesu atarejesha amani na furaha, ataondoa hofu, mashaka, kukata tamaa.


Isaya 61:1-2[1]Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu BWANA amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.

[2]Kutangaza mwaka wa BWANA uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao,

Mpokee Yesu maishani mwako ili upate uwezo wa kumteka shetani na Utapokea uwezo wa kumuamuru aondoke na ataondoka na hatakusumbua kamwe.. wakati ni huu wa kumkabidhi Bwana maisha Yako….


Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *