NENO ‘KAMSA’ LINA MAANA GANI KATIKA BIBLIA?

Maswali ya Biblia No Comments

Kamsa ni kelele zinazoashiria moto au vita (kwa kingereza kelele hizo huitwa battle cries)

Tusome baadhi ya vifungu,

Wimbo Ulio Bora 3:8[8]Wote wameshika upanga, Wamehitimu kupigana; Kila mtu anao upanga wake pajani Kwa hofu ya kamsa za usiku.

Sefania 1:15-18
[15]Siku ile ni siku ya ghadhabu,
Siku ya fadhaa na dhiki,
Siku ya uharibifu na ukiwa,
Siku ya giza na utusitusi,
Siku ya mawingu na giza kuu,


[16]Siku ya tarumbeta na ya kamsa,
Juu ya miji yenye maboma,
Juu ya buruji zilizo ndefu sana.


[17]Nami nitawaletea wanadamu dhiki, hata watakwenda kama vipofu, kwa sababu wamemtenda BWANA dhambi; na damu yao itamwagwa kama mavumbi, na nyama yao kama mavi.


[18]Fedha yao wala dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku ile ya ghadhabu ya BWANA; bali nchi yote pia itateketezwa kwa moto wa wivu wake; maana atawakomesha watu wote wakaao katika nchi hii, naam, ukomo wa kutisha.


Umeona hapo,ni vitabu vinavyoelezea siku ile kuu ambayo Bwana atakuja,utaona inafananishwa na siku ya kelele za vita ambazo huja ghafla. Wakati ule wana wa Israel waliuzunguka ukuta wa Yeriko kwa siku saba wakipiga kelele (kamsa) kuashiria vita inaanza. Na baada ya zile kelele ukuta wa Yeriko ukaanguka(Yoshua 5:1)

Yoshua 6:20-21[20]Basi watu wakapiga kelele, na makuhani wakazipiga tarumbeta; hata ikawa, hapo watu waliposikia sauti ya tarumbeta hao watu wakapiga kelele kwa sauti kuu sana, na ule ukuta wa mji ukaanguka nchi kabisa, hata watu wakapanda juu, wakaingia katika mji, kila mtu akiendelea kukabili mbele; wakautwaa huo mji.

[21]Basi wakaangamiza kabisa vitu vyote vilivyokuwa ndani ya mji, wanaume na wanawake, watoto na wazee, na ng’ombe, na kondoo, na punda, kwa makali ya upanga.

Na siku ya mwisho Yesu atashuka na malaika zake tarumbeta na kamsa itasikika kutoka mbinguni kuashiria mwisho umefika na hapo ndipo kila jicho litamuona waovu watalia kilio kikuu lakini hiyo haitasaidia kufuta uovu wao.

Tusitamani kuwepo wakati huo maana utakuwa wakati mbaya sana. Siku hiyo Bwana atawaangamiza waovu wote, kutakuwa ni kilio na kusaga meno…

Soma kitabu cha ufunuo sura ya 19 na 20 yote, uone jinsi waovu watakavyoangamizwa siku ile ya mwisho,


Wakati yote haya yanatokea Bwana atakuwa ameshafanya unyakuo wakaoshuhudia hayo ni wale ambao unyakuo umewaacha. Ndugu yangu ungama zambi zako wakati tulio nao ni wa siku za mwisho, siku za kamsa ya Mungu.

Shalom

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

  • Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *