Shalom watumishi wa Mungu. Karibu katika kujifunza Neno la Mungu ..
Maandiko yanaposema “….ASIJE MTU..” na si “… ASIJE SHETANI…” hii inatufunulia ya kwamba anayeitwaa taji ya mtu ni MTU. Hii ni kwasababu shetani mwenyewe taji hiyo haiwezi kumsaidia, ila mtu mwingine akiitwaa taji hiyo itamsaidia huko Aendako!
Tutafakari kwa UMAKINI ZAIDI
aliyeitwaa taji ya “yuda iskariote” alikuwa ni MTU aliyeitwa “Mathiya”. Baada ya yuda kushindwa kushikilia taji yake.
Tusome
Matendo ya Mitume 1:24-26
24″ Kisha wakaomba, wakasema, Wewe, Bwana, ujuaye mioyo ya watu wote, tuonyeshe ni nani uliyemchagua katika hawa wawili,
25 ashike mahali katika huduma hii na utume huu, alioukosa Yuda, aende zake mahali pake mwenyewe.
26 Wakawapigia kura; kura ikamwangukia Mathiya; naye akahesabiwa kuwa pamoja na mitume kumi na mmoja.”
Vilevile Aliyeitwaa taji ya ESAU ni MTU Yani nduguye YAKOBO
tunaona kilichopelekea pale ilikuwa tamaa ya chakula kimoja tu, ilimfanya esau kuipoteza taji ya urithi wa baraka za uzao wa kwanza.
Waebrania 12:16-17
16″ Asiwepo mwasherati wala asiyemcha Mungu, kama Esau, aliyeuuza urithi wake wa mzaliwa wa kwanza kwa ajili ya chakula kimoja.
17 Maana mwajua ya kuwa hata alipotaka baadaye kuirithi baraka, alikataliwa (maana hakuona nafasi ya kutubu), ijapokuwa aliitafuta sana kwa machozi.”
Unaposhindwa kuithamini nafasi yako, Mwingine ataichukua. Vilevile ukishindwa kuthamini huduma yako uliyopewa basi mwingine ataitwaa hivyo utapoteza thawabu zako.
• Umepewa huduma ya Uinjilisti, Uimbaji, Uchungaji, Maombezi n.k unapofanya kwa ulegevu Bwana anaweza kuitwaa kwako na kumpa mtu mwingine atakayeifanya kwa Viwango zaidi.
• Umepewa huduma ya kukirimu
(kusaidia Watumishi kwa ulivyo navyo) fanya kwa moyo maana ukizembea Bwana ataitwaa kutoka kwako kumpa mtu mwingine, Na taji yako UTAIPOTEZA
Mpendwa SHIKA SANA ULICHO NACHO! SHIKA SANA!!. Kina THAMANI KUBWA! na hakikisha unakizalia matunda usije ipoteza taji yako.
Maandiko yanatuambia majira tuliyopo shoka lipo kwenye mashina ya miti kukata mti USIOZAA!
Luka 3:9 “Na sasa hivi shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni.”
KUA MACHO! CHUKUA HATUA.
SHIKA SANA taji yako
Shalom
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.