FAHAMU TAFSIRI YA kumbukumbu 25:4 “Ng’ombe apurapo nafaka usimfunge kinywa”

Maswali ya Biblia No Comments

Bwana wetu yesu kristo Asifiwe. Karibu Tuyatafakari Maandiko matakatifu

Kwanza kabisa maana ya neno KUPURA ni ” Kutenganisha mbegu ya nafaka kutoka kwenye suke/ganda lake” Mfano tunapozitoa punje za nafaka (yaani ngano, mchele, maharage n.k) kutoka kwenye masuke yake hapo tunazipura Nafaka hizo

Zipo namna mbalimbali za Kupura nafaka, Kwa zama zetu mbinu maarufu zaidi inayotumika ni kutumia mashine lakini hapo Zamani watu walipura kwa kutumia watu au Wanyama.

Njia ya kutumia watu ilikuwa wanayatwaa masuke makavu na kuyatwanga au kuyachapa kwa fimbo nzito. Sasa njia hii ilikuwa ni ya kuchosha sana na ilitumia mda mrefu zaidi, hivyo watu walipendelea zaidi kutumia wanyama kama Ng’ ombe.

Ambapo Ng’ombe analazimishwa kupita juu ya masuke Yale makavu na anapoyakanyaga basi nafaka zile zinatenganika na masuke yake. Njia ilikubalika zaidi maana ilikuwa haiitaji nguvu, au watu wengi wala mda mrefu.

Sasa kulikuwako na tabia ya kuwafunga Ng’ombe kinywa wapurapo nafaka wakidai ni ili asile zile mbegu au nafaka zile alizozipura. Yaani mtu yu radhi Ng’ombe asipate japo punje kadhaa kati ya tani kadha wa kadha za nafaka alizopura kwa ajili yake!!. Hakika ni Ukatili! Sasa sababu ya kuzuka kwa tabia hii Mungu aliwapa amri wanaisraeli wasiwafunge vinywa Ng’ombe wapurapo Nafaka, Yaani waache nao wale kati ya kile walichokifanyia kazi

Kumbukumbu 25:4 “Ng’ombe apurapo nafaka usimfunge kinywa”.

JE! Kwanini Mungu anatoa Sheria hiyo? Hii ni kwasababu hata iweje Ng’ombe hawezi maliza tani nzima ya nafaka katika ghala lako, bali atakula punje kidogo ataacha. Hivyo haiwezi kukuletea athari Wala hasara yoyote katika shehena ya nafaka zako. Kutumia Ng’ombe kupuria nafaka inaonesha mzigo ulionao katika nafaka ni Mwingi. Hivyo kumnyima Ng’ombe kiasi Cha punje chache ambazo aanakula pale pale tu Wala haendi kutunza ghalani ni ukosefu wa UTU NA HURUMA.

Mithali 12:10 “Mwenye haki huufikiri uhai wa mnyama wake; Bali huruma za mtu mwovu ni ukatili.”

Kwa uweza wa Roho mtakatifu mtume Paulo anatoa Ufafanuzi wa mstari huu

Turejee.(Zingatia maandishi yenye herufi kubwa)

1 Wakorintho 9:9-14

9″ Kwa maana katika torati ya Musa imeandikwa, USIMFUNGE KINYWA NG’OMBE APURAPO NAFAKA Je! Hapo Mungu aangalia mambo ya NG’OMBE?

10 Au yamkini anena hayo kwa ajili yetu? Naam, yaliandikwa kwa ajili yetu; kwa kuwa alimaye nafaka ni haki yake kulima kwa matumaini, naye apuraye nafaka ni haki yake kutumaini kupata sehemu yake.

11 IKIWA SISI TULIWAPANDIA NINYI VITU VYA ROHONI, JE! NI NENO KUBWA TUKIVUNA VITU VYENU VYA MWILINI?

12 Ikiwa wengine wanashiriki uwezo huu juu yenu, sisi si zaidi? Lakini hatukuutumia uwezo huo; bali twayavumilia mambo yote tusije tukaizuia Habari Njema ya Kristo.

13 HAMJUI YA KUWA WALE WAZIFANYAO kazi za HEKALUNI HULA KATIKA VITU VYA HEKALU, NA WALE WAIHUDUMIAO MADHABAHU HUWA NA FUNGU LAO KATIKA VITU VYA MADHABAHU?

14 NA BWANA VIVO HIVYO AMEAMURU KWAMBA WALE WAIHUBIRIAO INJILI WAPATE RIZIKI KWA HIYO INJILI.”

Sasa katika mfano huo Ng’ombe anafananishwa na Mtumishi wa Mungu mwaminifu au kanisa la kristo. Hii inatufunulia kwamba kama kuna kanisa au Sehemu au Kupitia mtumishi Fulani wa Mungu unapata mafanikio makubwa kiroho na kimwili

JE! SI haki yake kupata vyovyote kati ya vile ulivyobarikiwa na Mungu? Mpendwa hupaswi kuzuia chochote ulichobarikiwa kwa Mtumishi au kanisa ambapo unapata mafanikio ya kiroho au hata kimwili, kwasababu HATAKUSABABISHIA HASARA! Bali atakula KIDOGO TU NA SI CHOTE.

Unaposaidiwa na Ng’ombe Kupura nafaka zako anachohitaji kama ujira wake ni kiasi kidogo tu Cha kukila pale anapofanya kazi na wala si ghala lako zima, utakuwa ni ukatili kiasi Gani kumnyima hata HICHO TU! ambacho kitampa nguvu ya kuendelea na kazi.

Hii inatuonesha pia utakuwa ni MTU wa aina gani, Kushindwa kujishika hata kidogo dhidi ya kanisa au mtumishi ambae kwake unapata baraka za Kimbinguni. Na biblia ndio iliyoamuru Wanaohubiri Injili wapate RIZIKI kupitia hiyo, Lakini unapoona ni mzigo sana kuchangia chochote hakika unazuia thawabu zako za mwilini na Rohoni pia Maandiko yanakuchukulia kama Mkatili na Mwovu (Mithali 12:10)

Kwa kutumia mfano huu halisi wa Ng’ombe apurapo nafaka inatueleza ni Ukatili namna Gani Kushindwa kuchangia kile Unachobarikiwa( mfano fedha ,Nguvu, muda n.k) Kufanya kazi ya Mungu iende mbele ilihali unanufaika nayo kwa kiasi kikubwa.

Pia unaweza rejea 1 Timoteo 5:18 kwa jambo Hilo.

Ndugu jitathamini JE! Wewe ni miongoni mwa Waovu na wakatili wanaofunga vinywa Ng’ombe wapurapo Nafaka!!? Kama wewe ni miongoni mwao basi TUBU ! Maana ulikuwa ukifanya DHAMBI! Na ugeuke njia zako kwa kuanza kumtolea Mungu na kuwa mtu anayejali, Mtolee Mungu kwa Moyo bila kulazimishwa Maana pumzi yake, Injili yake, Baraka zake n.k hutozwi chochote kuvipata. Sasa kwanini usijali kazi ya Mungu pasipo kusukumwa?!

Ubarikiwe sana.

Lakini Mpendwa kumbuka kristo anarudi na dalili zote zimeshatimia. Hivyo kama bado hujampokea Yesu maishani mwako fanya hivyo Leo na si kesho

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *