SWALI: ni kwanini biblia inakataza tusijiongezee HEKIMA, JE! Kuna ubaya gani kwa mkristro kuongeza maarifa au hekima?
JIBU :
tusome neno la Mungu kutoka Mhubiri 7::16
” Usiwe na haki kupita kiasi; Wala usijiongezee hekima mno; Kwani kujiangamiza mwenyewe?”
Hekima inayozungumziwa hapo sio hekima ile ya KiMungu tunayoifahamu, sio hiyo,bali hiyo pia hekima ya KiMungu tumeagizwa tuitafute sana,
Yakobo 1:5 “Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.”
Mithali 2:6 “Kwa kuwa Bwana huwapa watu hekima; Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu;”
Maandiko matakatifu yanamfananisha mtu mwenye hekima ya Ki-Mungu na mfanyabiashara ambaye biashara yake ni zaidi ya FEDHA!
Turejee
Mithali 3:13-15
13 “Heri mtu yule aonaye hekima, Na mtu yule apataye ufahamu
14 Maana biashara yake ni bora kuliko biashara ya fedha, Na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi.
15 Yeye ana thamani kuliko marijani, Wala vyote uvitamanivyo havilingani naye.”
Hivyo basi; Hekima inayozungumziwa na biblia takatifu katika kitabu Cha
Mhubiri 7::16b SI hekima ya kiMungu, Bali ni HEKIMA YA KIDUNIA. Ambapo hekima hiyo mbele za Mungu ni UPUUZI, kama isemavyo biblia katika 1Wakorintho 3:18
1 Wakorintho 3:18 “Mtu asijidanganye mwenyewe; kama mtu akijiona kuwa mwenye hekima miongoni mwenu katika dunia hii, na awe mpumbavu, ili apate kuwa mwenye hekima
19 MAANA HEKIMA YA DUNIA HII NI UPUUZI MBELE ZA MUNGU. Kwa maana imeandikwa, Yeye ndiye awanasaye wenye hekima katika hila yao.”
Kwa kuzingatia Maandiko hayo basi Hekima ya dunia hii ni upuuzi mbele za Mungu, Na mtu anapojiongezea sana hakika itamuangamiza! Tuwe makini wapendwa.
Mfano wa hekima za kidunia ni Ile inayosema “MWANADAMU ASILI YAKE NI NYANI” au “samaki asili yake ni majani yaliyodondokea majini”. Sasa hizi ni hekima au elimu za kidunia zilizoundwa na kuaminika miongoni mwa wasomi wengi ulimwenguni. Sasa mtu anayejikita zaidi katika hizo biblia inasema atajiangamiza mwenyewe!!.
Kwa maana atafikia mahali atasema hakuna Mungu!
Ndio Maana Maandiko yanatuasa tusijikite katika hekima hizo maana zimejaa upotovu Mwingi!
Bwana Atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.