Fahamu maana ya Mwanzo 32:24 ‘alimgusa panapo uvungu wa paja lake’

Maswali ya Biblia No Comments

Jibu:

Uvungu wa paja ni sehemu ya juu ya paja penye makutano ya mfupa wa paja na kiuno. Tunaona katika maandiko Yakobo akishindana na malaika usiku kucha na hakutaka kumuacha aondoke bila kumbariki. Malaika alipoona kuwa hamshindi akamtegua uvungu wa paja lake.

Tukumbuke kuna tofauti ya kuvunjika na kuteguka, kitu kinachovunjwa kinahitaji matengenezo mapya lakini kuteguka maana yake kitu/ kiungo fulani kimehama mahali pake kwa muda..

Kuna maeneo katika miili yetu ambayo yanamuunganiko wa mifupa miwili kama vile goti, bega, paja, viwiko vya mikono n.k maeneo haya yanaweza kupata hitilafu ya kuteguka.Mtu anapoteguka hupata maumivu makali na wakati mwingine huwa makali zaidi kama ya kuvunjika.

Sasa tujiulize kwa nini Yakobo aliteguliwa uvungu wa paja lake, kwa nini Mungu aliruhusu apate hayo maumivu, nini cha kujifunza katika hili?

Wana wa Mungu lazima tutambue kuwa baraka za Mungu haziji kwa wepesi, inatupasa kushindania na kukubali maumivu. Ukitaka baraka za Mungu kubali mapigo na maumivu….

Jina Israel lilipatikana kwa maumivu haikuwa rahisi tu likatokea, ukisikia baraka za Mungu zipo hapa usidhani ni kuchukua tu kuna gharama inatangulia…


Mfano wa maisha ya kubarikiwa ni kama huu….

Mathayo 6:38 “Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa”.

Bwana Yesu ndiye alisema maneno hayo

Kama ulichonacho hutaki kukitoa na unataka baraka kaa ukijua hakuna kitu utapata, ukiwa humtolei Mungu kwa kiwango cha kukupa maumivu ni vigumu kuziona baraka zake, sio kila wakati utaomba, unahitaji kufanya zaidi ya maombi,

Mtume Yohana alimwandikia Gayo waraka wa mafanikio,

1Yohana 1:2 “Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo”.

tujiulize kwa nini alimwandikia Gayo peke yake na si watu wote soma sura yote hiyo utaona mambo ambayo alijitoa kwa Mungu kwa njia ya kuwakaribisha wageni waliokuwa wanapeleka injili na sifa zake zikaenea katika kanisa. Hapo ndipo mtume Yohana alipomwandikia waraka ule wa kumtakia baraka. Halikuwa jambo jepesi kwa Gayo alijinyima nafsi yake kwa ajili ya wengine, kujitoa kwake kuliambatana maumivu nyuma yake…

Hivyo basi tujue kabisa kuwa ili kupata baraka za Mungu kuna kuteguliwa miguu yaani kuna mapambano, mapambano yetu sio kwa maneno bali matendo.


Bwana atusaidie katika mapambano hayo.

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *