Elewa nini maana ya neno gidamu katika biblia (Marko 1:7)

Maswali ya Biblia No Comments

Neno gidamu ni mikanda maalumu iliyotumika kwa ajili ya viatu, kipindi cha zamani viatu vilikuwa havina muoneakano kama wa sasa tunaouona,venyewe vilikuwa na utofauti, kwasababu viatu vya kipindi hichi vingi ni vya muundo wa kutumbukiza lakini vya zamani vilikuwa vinashikiliwa na mikanda ambayo huzungushwa kwenye miguu ili kufanya kiatu kisitoke miguuni, na hiyo mikanda inayoshikilia miguu ndio gidamu…

Tunalipata neno hili kwenye baadhi ya vifungu hivi,

Marko 1:7-8[7]Akahubiri akisema, Yuaja nyuma yangu aliye na nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuinama na kuilegeza gidamu ya viatu vyake.[8]Mimi niliwabatiza kwa maji; bali yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu.

Luka 3:16 “Yohana alijibu akawaambia wote, Kweli mimi nawabatiza kwa maji; lakini yuaja mtu mwenye nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuilegeza gidamu ya viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto”;

Mathayo 3.11 “Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto”.

Sasa ni Kwa namna gani Yohana aseme hastahili kulegeza gidamu ya viatu vya Yesu?

Kwa wakati huu na hata uliopita, shughuli ya kusafisha au kufungua viatu,ni kazi inayofanywa na watumwa wa chini sana, kwasababu inawalazimu kuchukua viatu vya bwana zao na kumvisha,kisha kumvua tena pindi atokapo katika shughuli zake,na kuvisafisha kuhakikisha vimekuwa visafi na kisha hurudi kwenda kumvisha tena bwana wake,na huwa ndo kazi yake anayoifanya siku zake zote..

Kwa desturi za wayahudi hawakuifanya hii kama ni kazi kwao au kwa mtumwa yoyote wa kiyahudi,kwa kuwa waliiona ni kazi ya kudharaulika,iliyojaa unyonge, hivyo ilifanywa sana na watu wa kaanani,mataifa mengine waliokuwa wanaishi Israel kwa kipindi hicho..

Hivyo Yohana kusema Maneno hayo kwamba hastahili kulegeza gidamu za viatu vya Yesu ni kuonyesha kutostahili kwake kuifanya kazi ndogo kama ile ya Yesu Kristo kwasababu aliutazama ukuu wa Yesu Kristo ulivyopita kiasi, akaona hata ile kazi ndogo sana iliyojaa kudharaulika kwa upande wake ni kubwa sana, hivyo alijiona hastahili kuifanya, hii inatuonyesha ni kujishusha kwa hali ya juu sana Yohana aliufanya kwa Bwana Yesu..

Hiyo inatufanya tuelewe ni kwanini Bwana alimfanya mtangulizi wake,na kumshuhudia kwamba Katika uzao wa Wanawake hakuwahi kutokea aliye mkuu Katika Ufalme wa Mbinguni kama Yohana,na hii yote ilitokea kwake kwasababu aliweza kuthamini na kupokea wito mdogo wa Bwana aliomwita..

Tujiulize na sisi je,tunaweza kuwa kama Yohana,ikiwa tutakuwa wazito kusafisha nyumba ya Bwana kwa kupiga tu deki, utaweza kufanywa mtangulizi? Jiulize kazi ndogo tu ya kusafisha maliwatoni utawezaje kutangulizwa?, Siri za ndani za ufalme wa Mbinguni utawezaje kuonyeshwa ikiwa utazidharau kazi zake ndogo..

Thamini kazi za Yesu(gidamu)

Shalom

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *