USIVITWAE VIUNGO VYA KRISTO NA KUVIFANYA VYA KAHABA.

Biblia kwa kina No Comments

Nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo.
Karibu tuyatafakari maneno ya uzima ya Bwana wetu Yesu Kristo.

Iko hatari kubwa sana katika nyakati hizi za Mwisho na kama tusipokuwa makini tutajikuta tunafanya kazi ya kuchosha. Na kwasababu ya upofu tukaona ni kawaida tu.

Wakristo wengi sana wanavitwaa viungo vya Kristo na kuvifanya kuwa vya kahaba(kuviungamanisha na viungo vya kahaba) tunapookoka miili yetu inakuwa ni hekalu la Roho Mtakatifu,  yaani Mungu mwenyewe anafanya makao ndani yetu. Sasa Wakristo wengi wanaliharibu hekalu la Roho Mtakatifu ambayo ni miili yao. Kwa kuutwa viungo vyao na kuviungamanisha ama kuvifanya kuwa ni vya kahaba.

1 Wakorintho 6:19
“Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; ”

Unaona hapo anasema miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu na anaongezea kwa kusema “….wala ninyi si mali yenu wenyewe.” Ndio maana huo mwili huhusiki na mapigo ya moyo yanavyopiga,wala hukusiki na kuziotesha nywele zako unapozinyoa yupo afanyaye hiyo kazi nae ni Mungu mwenyewe.

Kama maandiko yanavyosema.

1 Wakorintho 3:7
“Hivyo, apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye. ”

Sasa hebu tuutafakari kwa kina mistari hii michache kisha tutajua mwamini anavitwaaje viungo vya Kristo na kuwa vya kahaba?.

1 Wakorintho 6

¹⁵ Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha!

¹⁶ Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja.

¹⁷ Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye.
Unaona hapo mtume Paulo anawauliza “Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba?”


Tutakwenda kutazama ni kwa namna gani viungo vya Kristo Wakristo wengi wanavifanya viungo vya kahaba.

Tofauti na tunavyofikiri labda kuzini,ndio kuvitwaa viungo vya Kristo kuwa vya kahaba ndio lakini leo tutakwenda tukatazame kwa kina jambo moja hapa au mawili.

NI KWA NAMNA GANI TUNAVITWAA VIUNGO VYA KRISTO KUWA VYA KAHABA?.

MIZIKI YA KIDUNIA.

Ni kwa namna gani?,

leo hii Wakristo wengi utawasikia wakisema “Nimeokoka na ninampenda Yesu” lakini wakati huo huo kwenye simu yake ameweka nyimbo za injili lakini pia ana nyimbo za kidunia kwenye simu yake na anasikiliza nyimbo za injili akichoka anahamia nyimbo za kidunia. Na hapo unakuta anajua kuimba nyimbo za kidunia kuliko nyimbo za injili.

Na kinywa hicho hicho anachotumia kuimba nyimbo za kidunia zenye maudhui ya uzinzi asilimia 100, kinywa hicho hicho anakitumia kumuimbia Bwana na kumsifu na kuabudu.

Na mwili huo huo yaani HEKALU LA ROHO MTAKATIFU. Unauchezesha nyimbo za kidunia na mwili huo huo unauchezesha mbele za Bwana.

Haujui hapo unafanya ibada! Maana ibada inakamilishwa na sifa haijalishi ni ya Ki-Mungu au ya kishetani. Na unamtia Mungu hasira na wivu.

  1 Wakorintho 10:7
“Wala msiwe waabudu sanamu, kama wengine wao walivyokuwa; kama ilivyoandikwa, Watu waliketi kula na kunywa, kisha wakasimama wacheze. ”

Na kama ni Mkristo wa namna hii basi jua kabisa ile Nuru bado haijaangaza ndani yako maana siku zote giza haliwezi kuchangamana na nuru mahali palipo na giza Kuna ukosefu wa Nuru na mahali palipo na nuru hakuna giza.

Hivyo hivi vitu haviwezi kukaa pamoja hata siku moja haiwezekani. Usijidamganye wala kujitumainisha.

Miziki ya kidunia inakujenga nini na kukufundisha nini? Kama sio kukubomoa nafsi yako kila kukicha?.

Chagua ni wapi unaposimama huwezi kusimama pote haiwezekani ndugu yangu.

Unakaa na movie masaa 4, kila mtandao upo huna muda wa kuomba wala kusoma Neno upo upo tu ndugu nyakati hizi ni za uovu Kristo yupo mlangoni kurudi epuka kabisa.

Jikane nafsi yako leo kweli kweli futa miziki yote ya kidunia, movie zote.

Usidanganyike kumfata Kristo kweli kweli ni gharama sio lelemama ndugu. Ndio maana mwenyewe akasema mtu akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe ajitwike msalaba wake na anifuate. Jitwike msalaba wako usiangalie mambo ya ulimwengu huu yatakukosesha.

Bwana anaendelea kusema.

Luka 14
²⁸ Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia?

²⁹ Asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi, watu wote waonao wakaanza kumdhihaki,

³⁰ wakisema, Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza.

Piga gharama je unavyo vya kumalizia??kumfata Yesu Kuna gharama lazima uache vyote unavyovipenda sana sana, vinavyokinzana na mapenzi yake kisha ufuate kile anachotaka sio rahisi kama unavyodhani.

Amua leo utamuona Yesu mwenyewe akijidhirisha katika maisha yako na kukupa tumaini na hakikisho la Daima ndani yako na faraja na tumaini.

NGUO  ZISIZO NA HESHIMA NA MITINDO(Fashion)

suruali kwa mwanamke vinadhalilisha mwili wako kama mwanamke wa Kikristo kabisa. Na Hekalu la Roho Mtakatifu. Unapita huko wanaume wengi wanazini na wewe kwa kukuangalia na kukutamani. Mwanamume unavaa nguo zisizo na Heshima, unanyoa viduku (yaani unalidharau sana hekalu la Roho Mtakatifu) aliekwambia ukinyoa kawaida hutapendeza ni nani ama unatafuta attention ya wanawake? Ndugu yangu nyoa hicho kiduku vinginevyo utaangamia kabisa. Cheza na mambo mengine lakini usijaribu kulinajisi hekalu la Roho Mtakatifu.

Maranatha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *