YODI NI NINI KATIKA MAANDIKO?

Mitihani ya Biblia No Comments

Jibu: Tusome,

Mathayo 5:18 “Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie”.

Yodi ni neno lililotumika katika lugha ya Kiswahili cha zamani, lenye maana ya “herufi ndogo”.Kwa lugha ya kingereza ni small letter”.ndani ya sentensi yoyote kunakuwa na herufi kubwa na ndogo.. Zile ndogo huwa ndo Yodi…. Mfano mzuri tunaposema Yesu ni Mungu, Herufi kubwa hapo ni hiyo “Y” na “M” lakini hizo nyingine zote zilizosalia kama “e” “s” “u” “n” “i”  “u” ni YODI.

Hivyo Bwana Yesu alivyosema kwamba hakuna hata “yodi” moja wala nukta itakayoondolewa hata yote yatimie maana yake.. ni kwamba hakuna herufi yoyote (hata ile iliyo ndogo kuliko zote, ‘yodi’) itakayobadilishwa katika maneno ya torati, kwasababu maneno ya Mungu hayabadilii. Ndio maana ukianzia juu kidogo utaona anasema hakuja kuitangua torati bali kuitimiliza..

Mathayo 5:17 “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.

18 Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie”.

Mathayo 24:35 “Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe”.

Torati inaposema..

usizini”..Bwana Yesu hakuja kulibadilisha hilo andiko, bali alikuja kulitimiliza kwa kusema “mtu amtazamaye mwanamke amekwisha kuzini naye nafsini mwake”. Hapo hajaondoa chochote, bali ameongezea dawa. Torati inaposema “usiue” Bwana Yesu alisema “amwoneaye ndugu yake hasira hana tofauti na muuaji, hivyo itampasa hukumu tu kama muuaji”. Hapo hajaitangua wala kulibadilisha bali ameitimiliza, na sheria nyingine zote za kwenye torati ni hivyo hivyo..

Je bado unachuki na ndugu zako, maadui zako, ukijitumainisha kwamba wewe si muuaji?.ukijitumainisha kwamba wewe sio mzinzi??, bado unavaa nusu uchi,na suruali ukijitumainisha kwamba wewe si kahaba?? (kasome Mithali 7:10 ujipime kama wewe ni kahaba au la kwa mavazi yako),unajichua na kunatazama pornography ukijitumainisha kwamba wewe si mwasherati?, bado ni mshabiki wa mambo ya kidunia kuliko kitu kingine chochote ukijitumainisha kwamba wewe si wa kidunia??.

Kama unafanya mojawapo ya hayo, au yote, wakati wa kumkaribisha Mwokozi ndani ya maisha yako ni huu?..Usingoje kesho wala baadaye, saa ya wokovu ni sasa, na wakati uliokubaliwa ndio huu.. wakati wa kukimbilia Kalvari, Bwana akuokoe na kukutua mzigo ndio huu, sio kesho, kwasababu hujui kesho yako itakuwaje, labda leo ndio mwisho wako wa kuishi duniani, au leo ndio siku parapanda ya mwisho itakapolia, jiulize, unyakuo leo ukipita utakuwa wapi??.. Hivyo fanya uamuzi wa kumgeukia Yesu leo kwa kutubu dhambi zako zote kwake, na kwenda kubatizwa katika ubatizo wake wa maji tele (Yohana 3:23), na kwa jina la Yesu Kristo (Matendo 2:38), na Bwana atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu, atakayekuongoza katika kweli yote ya maandiko.

Pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Mafundisho zaidi, NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Maran atha.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *