Ebenezer/Ebeneza ni neno la Kiebrania lenye maana ya “Stone of Help” yaani JIWE LA Msaada.
Neno hili tunalipata katika kitabu cha 1 Samweli 4:1. Sehemu ambayo walikutanika wana wa Israeli kwenda kupigana na majeshi ya Wafilisti.
Na hata walipokutanika na kupanga vita Israeli walipokwenda kupigana na Wafilisti Israeli wengi yapata watu elfu nne walipigwa.
1 Samweli 4:2
“[2]Nao Wafilisti wakajipanga juu ya Israeli; na walipopigana, Israeli wakapigwa mbele ya Wafilisti; wakauawa watu wa jeshi lao lililokuwa uwandani wapata watu elfu nne.”
Na baada ya hapo wazee wa Israeli walikusanyika tena na kutafakari kwa nini wameshindwa vita vile? Wakatuma watu kwenda kulileta Sanduku la Bwana mahali kule liliko kuweko Shiro.
Na Israeli waliogopa sana wakamuomba wakamsihi sana Samweli awalilie kwa Bwana ili Bwana awasaidie maana walijua kabisa pasipo Bwana watakwenda kuangamizwa wote.
Na Baada ya Samweli kuwasikiliza alikwenda mbele za Bwana na Mungu akasikia akawatetea kwa kuleta ngurumo kubwa sana ambayo ilikwenda kuwadhoofisha kambi yote ya Wafilisti. Hivyo Israeli wakawapiga Wafilisti na wakazichukua sehemu zote ambazo Wafilisti walikuwa wamezichukua kutoka kwa wana wa Israeli.
Ndipo kwa tendo hilo ama kwa ushindi huo mtumishi wa Mungu nabii Samweli akachukua jiwe kubwa akalisikamisha kati ya Mispa na Sheni. Akaliita Ebenezeri/Ebeneza akasema “Hata sasa Bwana ametusaidia”.
1Samweli 7:12 Ndipo Samweli akatwaa jiwe, na kulisimamisha kati ya Mispa na Sheni, akaliita jina lake Eben-ezeri, akisema, Hata sasa Bwana ametusaidia.
Sasa Kwa nini Samweli alichukua jiwe na si kitu kingine kukisimamisha?
Samweli alitambua kwa kupata ufunuo kuwa aliewasaidia Israeli si mwingine Zaidi ya simba wa kabila la yuda nae ni Bwana wetu Yesu Kristo HALELUYA. Alijua yeye ndie alietoa ile ngurumo kama simba na kuwadhoofisha Wafilisti.
Warumi 9:33
“[33]kama ilivyoandikwa,
Tazama, naweka katika Sayuni jiwe likwazalo, na mwamba uangushao;
Na kila amwaminiye hatatahayarika.”
“HATA SASA MUNGU AMETUSAIDIA” kauli hii inaonyesha kabisa Samweli alitambua kuwa YESU KRISTO ndio Msaada wao siku zote na wakati wowote katika maisha yao.
Maana yake sio siku hiyo tu bali ni kila mara Mungu alikuwa pamoja nao.
Pia nikutundisha hata sisi watoto wa Mungu yaani tuliokombolewa kwa damu ya thamani ya Kristo Yesu. Tukiwa tumefunikwa na damu yake ambayo wakati wowote anatulinda maana uhai wetu umefichwa katika Kristo Yesu. Wala hakuna mwingine aweza kututoa na kutuangamiza katika mikono yake HALELUYA.
Mkabidhi sasa Kristo Yesu maisha yako afanyike kuwa Ebenezeri katika maisha yako na si hivyo tu bali apate kukupa uzima wa milele bado hujachelewa unayo nafasi ndugu yangu.
Shalom.
Tafadhali washirikishe na wengine ujumbe huu.
Pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Mafundisho zaidi, NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618