Dhamiri ni nini?

  Uncategorized

Bwana Yesu asifiwe!

Dhamiri au Dhamira. Ni hisia za ndani kabisa zinazomsaidia Mtu kupambanua jema na baya. Na hii haitokani na kufundishwa lakini Mungu kakiweka ndani yetu.

Dhamiri ni mfano wa mtu wa ndani ambae yeye anatusahihisha na kutushuhudia pale tunapotaka kufanya jambo lisilopaswa kama uovu nk. Hivyo wakati mwingine utakuta unakosa furaha au Amani pale unapotaka kufanya jambo fulani ambalo wakati mwingine kwa akili za kawaida linaweza kuonekana ni jema lakini dhamiri inapotushuhudia haijalishi jambo hilo tunaona linafaida ama ni zuri kiasi gani inatupasa kuacha mara moja.

Tusiwe watu wa kushindana na dhamiri zetu maana siku zote dhamiri haisemi uongo ni kama shahidi ama muwakilishi wa Mungu kwa tuliookoka na kwa wala ambao hawajaokoka.

Mfano mtu anapotaka kuiba,kubaka,kuua, dhamiri inamshuhudia ndani yake kuwa hicho kitu si sawa pasipo hata kuambiwa na mtu ama kuhubiliwa ila ghafla tu dhamiri itaanza kumshuhudia.

Tukisoma Biblia neno hili “Dhamiri ” limeonekana mara kadhaa ambapo tutakwenda kuona mfano ule ambao Mafarisayo na Waandishi walipomkamata yule mwanamke katika uzinzi na wakamuuliza Yesu kwa unafiki wakijua kabisa torati inasema apigwe mawe mpaka kufa kuondoa uovu lakini Bwana Yesu aliwaambia maneno ambayo dhamiri zao wote ziliwachoma wakubwa kwa wadogo wakaondoka wakamuacha yule Mwanamke wasimpige mawe.

Yohana 8:3  “Waandishi na Mafarisayo wakamletea mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, wakamweka katikati.

4  Wakamwambia, Mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini.

5  Basi katika torati, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake namna hii; nawe wasemaje?

6  Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika nchi.

7  Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe.

8  Akainama tena, akaandika kwa kidole chake katika nchi.

9  Nao waliposikia, WAKASHITAKIWA NA DHAMIRI ZAO, wakatoka mmoja mmoja, wakianzia tangu wazee hata wa mwisho wao; akabaki Yesu peke yake, na yule mwanamke amesimama katikati.

10  Yesu akajiinua asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia, Mwanamke, wako wapi wale washitaki wako? Je! Hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia?

11  Akamwambia, Hakuna, Bwana. Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena.Dhamiri siku zote inasema ukweli ili kuzilekebisha njia zetu.

Na Biblia imetabiri katika nyakati za Mwisho (Fahamu tunaishi katika nyakati za Mwisho nazo ndizo hizi tulizopo mimi na wewe unaesoma ujumbe huu.)

Kuwa watatokea watu wasemao uongo na ijapokuwa dhamiri zao zitawashitaki lakini hawatataka kuzisikiliza watataka kutimiliza uovu wao.

1Timotheo 4:1  “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;

2  kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;

3  wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli”

Soma pia

Warumi 2:15, Warumi 9:1.

Ikiwa Kuna mambo unafanya na dhamiri yako inakushududia kuwa si sawa basi acha mara moja na dhamiri yako I hai haijafa lakini kama unaona unafanya maovu na huoni dhamiri ikikushitaki basi  jua dhamiri yako imeshakufa na Unamuhitaji Kristo Yesu ili aihuishe tena na na akuhuishe na wewe pia kwa damu yake ili upate kuurithi ule uzima wa milele tulioahidiwa katika Kristo Yesu.

Shalom.

Pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Mafundisho zaidi, NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

LEAVE A COMMENT