NINI MAANA YA KUSAGA MENO?

Maswali ya Biblia No Comments

Kusaga meno ni kitendo cha kunga’ta meno kwa nguvu , kutokana na maumivu na uchungu fulani fulani..mtu aliyejikata na kisu au kujikwaa kwenye kidole utaona atang’ata meno kwa nguvu kutokana na maumuvi anayoyasikia au uchungu au hasira fulani (Soma Matendo 7:54).

wakati mwingine mpaka kung’ata huku yanasuguana. Sasa kitendo hicho ndicho kinachoitwa kusaga meno.

Katika Maaandiko kuna sehemu mbalimbali zimezungumzia tendo hilo la kusaga meno, utaona Bwana Yesu alipozungumzia juu ya mateso yaliyopo Jehanum hakuacha kuhusisha tendo la usagaji wa meno. Ikifunua kuwa Jehanamu sio mahali pa raha. Bali pa mateso makali sana

Mathayo 13:41  “Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka katika ufalme wake machukizo yote, na hao watendao maasi,

42  na kuwatupa katika tanuru ya moto, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno”.

Mathayo 25:30 “Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno”. 

Vifungu vingine vya biblia vinayofanana na hivyo, inayozungumzia kitendo cha kusaga meno ni pamoja na Zaburi 37:12, Mathayo 8:12, Mathayo 13:50. Mathayo 22:13, 25:30, Marko 9:18 na Luka 13:28.

Hayo yote yanaonyesha ukali wa mateso yaliyopo Jehanum. Kwamba si sehemu nzuri, kutakuwa na maumivu makali na mateso kwa wale wote ambao hawajampokea Kristo na waliorudi nyuma.

Kama hujampa Yesu Kristo maisha yako, ni vyema ukafanya hivyo kabla muda wako wa kuishi duniani haujaisha. Unachopaswa kufanya ni kutubu tu mahali ulipo. Unatubu dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kisha unatafuta ubatizo sahihi wa maji tele na kwa jina la YESU KRISTO kulingana na Matendo 2:38. Kwa ajili ya kukamilisha wokovu wako.

Na kama ulishabatizwa katika vigezo hivyo hapo juu basi hauhitaji kubatizwa tena. Na mwisho kabisa Bwana mwenyewe atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu atakayekusaidia kushinda dhambi.

Bwana akubariki.

Pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Mafundisho zaidi, NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Tafadhali share na wengine.

Kwa Maombezi, Ushauri Maswali Wasiliana nasi kwa namba hii 255693036618

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *