Je kinga kilichotolewa motoni kinafunua Nini kibiblia

  Maswali ya Biblia

Jambo hili tunaliona katika kitabu cha zekaria 3:2 Yoshua akiambiwa Yeye ni kinga kilicho tolewa motoni, hiyo kinga ilikuwa ni kitu gani?

Kinga ni kama kijiti, kwahiyo tunaposema kinga Cha moto, inamaanisha kijiti Cha moto, na habari hii tunaipata Kwa Yoshua aliyekuwa kuhani mkuu wakati pale alipokuwa amesimama mbele za Mungu tunaona wakati huo na shetani alikuwa amesimama in pembeni yake kumsitaki Yoshua, lakini pale palikuwa na malaika aliyemwambia shetani “Bwana akamwambia Shetani, Bwana na akukemee Ewe Shetani; naam, Bwana, aliyechagua Yerusalemu, na akukemee; JE! HIKI SI KINGA KILICHOTOLEWA MOTONI?

tusome habari hiyo

Zekaria 3:1 “Kisha akanionyesha Yoshua, kuhani mkuu, amesimama mbele ya malaika wa Bwana, na Shetani amesimama mkono wake wa kuume ili kushindana naye.
2 Bwana akamwambia Shetani, Bwana na akukemee Ewe Shetani; naam, Bwana, aliyechagua Yerusalemu, na akukemee; JE! HIKI SI KINGA KILICHOTOLEWA MOTONI?
3 Basi, Yoshua alikuwa amevaa nguo chafu sana, naye alikuwa akisimama mbele ya malaika.
4 Naye huyo akajibu, akawaambia wale waliosimama mbele yake, akisema, Mvueni nguo hizi zenye uchafu. Kisha akamwambia yeye, Tazama, nimekuondolea uovu wako, nami nitakuvika mavazi ya thamani nyingi”.

Lakini ukisoma hiyo habari, hapo malaika alimaanisha hicho kinga kilichotolewa kwenye moto ilikuwa ni Yerusalemu na hakumaanisha Yoshua, maana tangu Israeli imwasi Mungu Kwa maovu yake kwa kutomkubari masihi, na kwa kutenda mambo yaliyo kinyume na maagizo ya Mungu aliufanya mji huo wa Yerusalemu uteketee kabisa, lakini Kwa Mungu ni wa Rehema, Mungu anakuja kuukoa tena japo kuwa ulikuwa tayari umeteketezwa milele lakini akaamua kuumboa tena, ni mfano wa kijiti chochote kikiingia katika moto ni lazima kiteketee tu, lakini hapa Mungu anaonyesha Upendo wake japo mji huo ulikuwa katika kupotea lakini akauokomboa

Ndiyo maana hata ukisoma baadhi ya maandiko utaona jinsi Mungu alivyo kuwa anaungamiza mji kutokana na uovu wao

Amosi 4:7 “Tena nimeizuia mvua msiipate, ilipobaki miezi mitatu kabla ya mavuno; nami nimenyesha mvua juu ya mji mmoja, nikaizuia mvua isinyeshe juu ya mji mwingine; sehemu moja ilipata mvua, na sehemu isiyopata mvua ilikatika.
8 Basi kutoka miji miwili mitatu walitanga-tanga kuendea mji mwingine wapate kunywa maji, wasipate ya kuwatosha; lakini hamkunirudia mimi, asema Bwana.
9 Nami nimewapiga kwa ukavu na koga; wingi wa bustani zenu na mashamba yenu ya mizabibu, na mitini yenu na mizeituni yenu imeliwa na tunutu; Lakini hamkunirudia mimi, asema Bwana.
10 Nimewapelekea tauni, kama tauni ya Misri; vijana wenu nimewaua kwa upanga, na farasi wenu nimewachukulia mbali; nami nimeupandisha uvundo wa matuo yenu na kuuingiza katika mianzi ya pua zenu; lakini hamkunirudia mimi, asema Bwana.

11 Baadhi yenu nimewaangamiza, kama hapo MUNGU ALIPOIANGAMIZA SODOMA NA GOMORA, NANYI MKAWA KAMA KINGA KILICHONYAKULIWA MOTONI; LAKINI HAMKUNIRUDIA MIMI, ASEMA BWANA.

Jambo hili linatukumbusha kwetu pia, ni mambo yamekuwa yakizuka, lakini katika hayo tumeona Mungu akituvusha, na kutukomboa, tuangalie ngojwa kama CORONA, RED EARS( Macho mekundu)nk.. Haya ni baadhi lakini ukiangalia ni Mungu alituvusha katika kuagamia huko kutoka katika kijiti kilicho ndani ya moto..

Tusiudharau mwema wa MUNGU ambao anatuonyesha, na anafanya hivi ili kutukumbusha kuacha maovu yetu na kumrudia Bwana, lakini kama tukishindwa kumuheshimu wema wa MUNGU hakika tutangamia milele

Ikiwa ulikuwa bado ujampa Yesu Kristo maisha yako basi Leo Mwamini naye atakukomboa, kumbuka duniani tunapita kama ukishindwa Leo kutengeneza hapa, basi tambua huko hakutakuwa na nafasi Tena

Kwa Maombezi/Maswali/ Ratiba za Ibada Wasiliana nasi Kwa namba

+225789001312/ +225693036618

Pia unaweza kujiunga na channel yetu ya mfundisho ya NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

LEAVE A COMMENT