TUNGUJA NI NINI?

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom…

Huu ni aina ya mmea ambao haupatikani kirahisi sana, na tabia nyingine ya mmea huu, unakuwa na maumbile kama ya mtu,

Na maumbile ya mzizi wa mmea huu hufanana na maumbile ya mwili wa mwanadamu, ndo mana ilifika wakati hata watu wazamani hata sasa baadhi yao, huwa na imani kuwa mmea huu una nguvu za ki-Ungu ndani yake

Kwa imani kama hiyo ilipelekea mpaka wachawi na wasio wachawi kuanza kuitumia Katika kazi zao.. mfano, ni mti wa muarobaini jinsi unavyotumika kwa Matumizi mbalimbali..

Katika Maaandiko tunamwona mwanaamke mmoja anayeitwa Reheli, ambaye aliamini mizizi ya mmea huu, “tunguja ” unaweza kumpatia Mtoto kwa kipindi fulani…

Kwa kuamini kwake hivyo ilifika wakati Mtoto wa dada yake ambaye ni Rubeni, alipouona mmea huu shambani na kuchukua mizizi kwa kusudi la kumpelekea mama yake (lea) yeye Reheli alipomuona Rubeni alikimbia moja kwa moja kwa dada yake kwenda kumwomba baadhi ya mizizi ya tunguja hizo ili zimsaidie kupata uzao..

Lakini tunakuja kuona Lea alikataa kumpa mizizi hiyo mpaka kupelekea Raheli kuuza zamu yake ya kulala na mume wake, Yakobo” na hiyo yote ni kwasababu Raheli alikuwa na matamanio makubwa ya kupata Mtoto akaliondoa tumaini lake lote kwa Mungu na kulipeleka kwenye zile tunguja akiamini zitamsaidia kupata Mtoto..na hivyo kuuza haki yake ya kukutana na mumewe na kumpa dada yake, (Ni kama vile Esau alivyouza haki ya mzaliwa kwa kwanza kwa ndugu yake Yakobo kwa chakula cha dengu)

Na matokea ya Raheli kufanya vile hayakuwa mazuri kwasababu dada yake alikuja kupata watoto wengine watatu, na yeye hakupata Mtoto…

Tusome,

Mwanzo 30-15:21

15 Naye akamwambia, Je! Ni jambo dogo kuninyang’anya mume wangu; hata wataka kuzitwaa tunguja za mwanangu pia? Raheli akamwambia, Kwa hiyo atalala kwako usiku huu kwa tunguja za mwanao


[16]Yakobo akaja kutoka kondeni jioni, Lea akatoka kumlaki, akasema, Lazima uje kwangu, kwa sababu nimekuajiri, kwa tunguja za mwanangu; akalala kwake usiku ule.


[17]Mungu akamsikia Lea, naye akapata mimba, akamzalia Yakobo mwana wa tano.


[18]Lea akasema, Mungu amenipa ujira wangu, kwa sababu nimempa mume wangu mjakazi wangu. Akamwita jina lake Isakari.


[19]Lea akapata mimba tena, akamzalia Yakobo mwana wa sita.


[20]Lea akasema, Mungu amenipa mahari njema, sasa mume wangu atakaa nami, kwa kuwa nimemzalia wana sita. Akamwita jina lake Zabuloni.


[21]Baadaye akazaa binti, akamwita jina lake Dina.

Inatufundisha nini?

Ahadi za Mungu siku zote ni thabiti, alichokisema au alichokiahidi lazima akitimize..

Lakini tunaposhindwa kuwa na uvumilivu na kuamua kutafuta njia nyingine mbadala ili kupata jambo ambalo Mungu tayari alishatuahidi na kutuambia tungoje, basi tunajipoteza wenyewe na ndivyo tunavyozidi kukikawisha kile kitu kufika kwa wakati..

Yamkini siku ile Yakobo alipotoka shambani ndo ilikuwa siku ya Raheli kupata ujauzito , lakini kwa udanganyifu wa shetani aliomshawishi akamwamisha imani yake kwenda kwenye mizizi wanayoitumia watu wasio mjua Mungu, mwishowe Mungu akamsikia dada yake badala yake , ikamfanya kusubiri miaka mingi bila uzao mpaka huruma za Mungu zilipomjilia…

Ikiwa na wewe upo Katika njia hii, unatafuta uzao, Bwana amekuahidi atakupa Mtoto, usianze kutanga tanga kwa waganga wa kienyeji , Vumilia, kuwa mtu wa subira, kutanga tanga hakufanyi uharakishe kupata uzao wako uje badala yake ndo unauchelewesha kabisa..

Na vingine vingi kama mali, afya n.k” hatuvipati kwa waganga au kupiga ramli na matambiko bali tunayapata yote kwa kuzishikilia ahadi za Mungu, Kuziamini na kuziishi..

Je umeokoka?, ikiwa bado muda ndo huu, hakuna tumaini lingine nje ya Yesu Kristo, Saa ya Wokovu Ndio sasa..

washirikishe na wengine habari hizi njema Kwa kushea , au wasiliana nasi kwa namba hii 255693036618

Pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Mafundisho zaidi, NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *