THENASHARA NI NINI?

Maswali ya Biblia No Comments

Thenashara ni neno la kiebrania linalomaanisha, namba kumi na mbili” badala ya kusema watu kumi na 12 unaweza kusema watu tenashara , au kusema miezi kumi na 12, ukasema miez tenashara, makabila kumi na 12 ni sawa na kusema makabila tenashara “‘ n.k’

Biblia imelitumia Neno hilo Thenashara kuwakilisha wale Wanafunzi 12 wa Bwana Yesu, ambao baadaye waliitwa Mitume..

Marko 3:16  “Akawaweka wale Thenashara; na Simoni akampa jina la Petro;

17  na Yakobo, mwana wa Zebedayo, na Yohana nduguye Yakobo, akawapa jina la Boanerge, maana yake, wana wa ngurumo;

18  na Andrea, na Filipo, na Bartholomayo, na Mathayo, na Tomaso, na Yakobo wa Alfayo, na Thadayo, na Simoni Mkananayo,

19  na Yuda Iskariote, ndiye aliyemsaliti. Kisha akaingia nyumbani”

Na ni kwanini wanafunzi hawa 12, watenganishwe kwa kuitwa hivyo Thenashara?.. Ni kwasababu Bwana Yesu alikuwa anao wanafunzi wengine wengi zaidi ya 70,

Luka 10:1 “Basi, baada ya hayo Bwana aliweka na wengine, sabini, akawatuma wawili wawili wamtangulie kwenda kila mji na kila mahali alipokusudia kwenda mwenyewe.”

hivyo ili kuwatofautisha hawa wanafunzi 70 na wale 12 aliowateua kwanza ndio likatumika hilo neno “Thenashara”

Unaweza kulisoma neno hilo pia katika Mathayo 26:14-16, Marko 4:10, Marko 9:35, na Yohana 20:24

Je umefanyika kuwa Mwanafunzi wa Yesu? kwa kutubu dhambi zako zote, na kumaanisha kuziacha na vile vile kuchukua msalaba wako na kumfuata yeye?

Luka 14:27  “Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu”

Maran atha!

Pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Mafundisho zaidi, NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *