UCHAGA NI NINI?

Maswali ya Biblia No Comments

Jibu: Tusome,

Luka 12:24 “Watafakarini kunguru, ya kwamba hawapandi wala hawavuni; hawana GHALA wala UCHAGA, na Mungu huwalisha. Bora ninyi mara nyingi kuliko ndege!”

Uchaga” ni jengo kubwa lililotengenezwa kwaajili ya kuhifadhia nafaka pamoja na aina nyingine ya vyakula vya mifugo na binadamu, tofauti na “ghala….ghala ni chumba/nyumba ndogo ya kuhifadhia nafaka, lakini..

Bwana Yesu aliposema, tuwatafakari kunguru, kwamba hawana “Ghala” wala “Uchaga”, alimaanisha kunguru hawana mahali pa kuhifadhia chakula kwaajili ya vipindi vigumu vinavyokuja mbele yao ijapokuwa hawana sehemu za kuweka akiba za chakula msimu wa kiangazi lakini hawafi kwa njaa na wanaishi!!!!

Ukitafakari kisa cha zamani cha nabii Eliya , kipindi ambacho Mungu alifunga Mbingu kwa miaka mitatu , ni kipindi ambacho watu na wanyama walikufa kwa kukosa chakula, lakini utaona kunguru bado walikuwa wanaishi na wanakula vizuri hata Mungu kuwatumia hao kumpelekea chakula mtumishi wake…

1Wafalme 17:2 “Neno la Bwana likamjia, kusema,

3 Ondoka hapa, geuka, uende upande wa mashariki, ujifiche karibu na kijito cha Kerithi kinachokabili Yordani.

4 Itakuwa utakunywa maji ya kile kijito; NAMI NIMEWAAMURU KUNGURU WAKULISHE HUKO.

5 Basi akaenda akafanya kama alivyosema Bwana; kwa kuwa akaenda akakaa karibu na kijito cha Kerithi, kinachokabili Yordani.

6 KUNGURU WAKAMLETEA MKATE NA NYAMA ASUBUHI, na mkate na nyama jioni, akanywa maji ya kile kijito”.

Umeona?.. wakati watu wanakufa kwa njaa, Kunguru na Watoto wao wanakula mpaka wanasaza, mpaka wanakuwa na akiba ya kumpelekea Eliya, mtumishi wa Mungu.

Lakini sasa Bwana Yesu anakuja kusema katika Luka 12:24, kwamba TUWATAFAKARI HAO!!.. Kama Baba wa mbinguni anawapa chakula hao, na ijapokuwa hawana maghala wa uchaga, si Zaidi sisi endapo tukimwamini na kumtegemea yeye?.. Kwasababu sisi ni bora kuliko kunguru mara nyingi.

Baba yetu anatuhurumia sisi mara nyingi Zaidi, kuliko anavyowahurumia kunguru!. Tunapomtegemea yeye, hata kama tutapitia hali ngumu na za ukame kiasi gani, basi Bwana Yesu hatatuacha tupungukiwe kabisa…atakuwa na sisi na kutuhudumia kuliko anavyowahudumia kunguru..

Waebrania 13:5 “Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa.

6 Hata twathubutu kusema, Bwana ndiye anisaidiaye, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?”

Je umempokea Yesu leo?, je umefanyika mtoto wake?, kama bado kumbuka dunia si salama, wala haina mshahara wowote Zaidi ya mauti, dunia itakususha thamani Zaidi ya kunguru siku ya mateso, kipindi cha Eliya wote waliokuwa wanaitumainia dunia, walikufa kwa njaa, lakini kunguru wakawa wanaishi…wote waliokuwa wanaabudu mabaali waliangamia, lakini kunguru waliishi!..Lakini waliomtegemea Mungu waliishi na kudumu,

Mpokee Yesu leo kama bado hujampokea, pia ukabatizwe katika ubatizo sahihi kwaajili ya ondoleo la dhambi na upokee kipawa cha Roho Mtakatifu.

Maran atha!

Pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Mafundisho zaidi, NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *