SHETRI NI NINI?

Maswali ya Biblia No Comments

Jibu: Tusome,

Marko 4:35 “Siku ile kulipokuwa jioni, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng’ambo.

36 Wakauacha mkutano, wakamchukua vile vile alivyo katika chombo. Na vyombo vingine vilikuwako pamoja naye

37 Ikatokea dhoruba kuu ya upepo, mawimbi yakakipiga chombo hata kikaanza kujaa maji.

38 Naye mwenyewe alikuwapo katika SHETRI, amelala JUU YA MTO; wakamwamsha, wakamwambia, Mwalimu, si kitu kwako kuwa tunaangamia?”.

Katika Habari hiyo tunaona Wanafunzi walimchukua Bwana Yesu kama alivyo (yaani bila ya kitu chochote cha njiani kama vile chakula, au mavazi)... Na kumchukua kunakozungumziwa hapo ni kumchukua, kama vile mtu anavyomchukua mwenzake na kumpa lifti ya gari, ndivyo wanafunzi walivyomchukua Bwana Yesu..

tunaona walipokuwa njiani ndani ya ile Merikebu, Bwana Yesu alienda kulala katika Shetri ya Merikebu.

SHETRI” au kwa lugha nyingine “TEZI”, ni sehemu ya Nyuma ya Meli au Merikebu, ambayo ni pana, na ndiyo iliyotumika katika kuwekea mizigo, na pia ndipo palipotengenezewa vyumba vya kulala watu. Sehemu ya mbele ya Meli au Merikebu inaitwa “OMO”, ambayo ni nyembamba ili kuisiaidia meli kukata mawimbi.

Bwana Yesu alienda kulala kwenye Shetri ambako kulikuwa na Nafasi ya kulala na kulala juu ya mto, Mto unaozungumziwa hapa sio mto wa kutiririsha maji, bali ni ule mto wa kulalia kitandani, kuupatia shingo egemeo bora).. Na akiwa Katika usingizi, dhoruba ikaanza chombo kikakaribia kuzama wanafunzi wakamwamsha Bwana na Bwana Yesu akaikemea ile Dhoruba ikatulia..

kikubwa tunachoweza kujifunza katika tukio hilo ni kuwa, Bwana Yesu anaweza kuwa yupo ndani yetu lakini amelala!. Tusipopaza sauti zetu kwa nguvu kwa maombi, basi tutahangaika na Dhoruba zilizopo nje, na wala yeye hatasema chochote..

Hii inatukumbusha kuwa waombaji, na si waombaji tu, bali waombaji wenye bidii, wenye kupaza sauti mpaka majibu ya maombi yatokee.

Bwana atusaidie katika hayo.

Pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Mafundisho zaidi, NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *