Kupiga ramli ni nini katika Biblia ?

  Maswali ya Biblia

Ramli ni elimu ya ufalme wa giza, ambayo waganga, wachawi na wenye mapepo ya utambuzi huwa wanatumia katika kutabiri mambo yajayo, basi mtu yeyote anayetumia njia hiyo au elimu hiyo kutabiri mambo yajayo, mtu huyo anajulikana kama mpiga ramli na huwa wanatumia viganja vya mikono au viungo vya wanyama kupiga ramli zao. ili kutabiri jambo la mtu litakalo tokea mbeleni

Na jambo hili tunaweza kuliona hata katika agano la kale

2Wafalme 17:16
“Wakaziacha amri zote za Bwana, Mungu wao, wakajifanyizia sanamu za kusubu, yaani, ndama mbili, wakafanya na Ashera, wakaliabudu jeshi lote la mbinguni, wakamtumikia Baali.

17 Wakawapitisha watoto wao, waume na wake, motoni, WAKAPIGA RAMLI, wakafanya uchawi, wakajiuza nafsi zao wapate kufanya yaliyo maovu machoni pa Bwana, hata kumkasirisha.

18 Kwa hiyo Bwana akawaghadhibikia Israeli sana, akawahamisha mbali na uso wake; wala hapana aliyesalia ila kabila ya Yuda peke yake

19 Hata na watu wa Yuda hawakuyashika maagizo ya Bwana, Mungu wao, lakini walikwenda katika amri za Israeli walizokuwa wamezifanya wenyewe.

20 BASI BWANA AKAKIKATAA KIZAZI CHOTE CHA ISRAELI, AKAWATESA, NA KUWATIA KATIKA MIKONO YA WATU WENYE KUWATEKA NYARA, HATA ALIPOKWISHA KUWATUPA, WATOKE MACHONI PAKE”.

Jambo hili halikuwa agizo la Bwana watu wapige ramli, ndiyo maana tunaona Bwana akighadhibika Kwa kutokutii Kwao., japo wengine walikubali kuacha, na baadhi walikataa, Hadi iliwapelekea kupelekwa katika nchi ya utumwa ashuru na babeli, na kutolewa katika nchi yao, hiyo ilikuwa ni kwa sababu ya kutokutii kwako.

Je ni kweli mtu akienda Kwa mganga ili apigiwe ramli Kwa ajili ya kujua kesho yake, je ni kweli atatabiriwa mambo ya ukweli?

Si kweli kabisa jambo hili, shetani hana uwezo hu wowote wa kujua kesho itakuwaje, sawa sawa na wanadamu jinsi alivyo hana uwezo wa kujua kesho kutatokea nini, mwenye UWEZO WA KUJUA MAMBO YA KESHO NA YAJAO NI MUNGU PEKEE NA NDIYO MAANA ANAJULIKANA KAMA ALFA NA OMEGA , (MWANZO NA MWISHO)

Lakini shetani anachoweza kufanya ni kupanga jambo leo ambalo anatumaini kuwa kesho litatokea. Kwahiyo mtu anayekwenda kwa mganga, akitaka kujua kesho yake itakuwaje..shetani atakachokifanya ni kumpangia huyo mtu kesho yake, jinsi itakavyokuwa.

Mfano unakuta mtu anakwenda Kwa mganga, ili kutaka kujua kama kesho atatembelewa na wageni au la!.. na yule mganga akamtabiria na kumwambia kwamba kesho atatembelewa na wageni, na tena akawataja na majina, na muda watakaokuja.. Na kweli kufikia hiyo kesho, hao wageni wakaja kama alivyotabiriwa jana.

Sasa hapo sio kwamba huyo mganga, kimiujiza kapelekwa kesho na kuona matukio yake. Bali anachokifanya ni kutuma mapepo, ambayo yatakwenda kuwaingia hao watu aliowataja na kuwashawishi wamtembelee huyo mtu katika huo muda aliopanga yeye siku ya kesho.

na ikiwa hao wageni hali zao za kiroho si nzuri, inakuwa rahisi wao kuvamiwa na mapepo hayo, wanajikuta wanaenda Kwa huyo mtu.

Kwahiyo wote wanaopiga ramli, ndio kitu wanachofanyiwa na shetani (wanatengenezewa matukio) pasipo wao kujua, wakidhani wanaambia mambo yajayo. Hiyo ndio sababu Bwana aliwakataza na anatukataza Watoto wake hata leo, tujiepushe na Ramli na aina yoyote ile pamoja na ushirikina, kwasababu zinaasisiwa na shetani, baba wa Uongo. (Yohana 8:44).

Shetani angekuwa anajua mambo yajayo (future), basi angejua hata siku ya unyakuo ni lini, lakini hajui chochote!. Anachojua kiufasaha ni mambo yaliyopita tu!, kwasababu tayari ni matukio ambayo yameshatokea, jambo ambalo pia lipo ndani ya uwezo wetu sisi wanadamu kujua mambo yaliyopita, lakini si kujua mambo yajayo.

Kwahiyo unapokwenda kwa mganga kupiga ramli kutaka kujua kesho yako, fahamu kuwa ni umeenda kwa shetani kutengenezewa kesho yako na si kuambiwa kesho yako, Utatengenezewa vifo na shetani, utatengenezewa mikosi, na shida, na vile vile utatengenezewa baraka bandia ambazo mwisho wake ni laana.

Sasa ni wapi penye salama ya maisha yako, salama ya maisha yako utaipata Kwa Mungu pekee na wala si kwa wanadamu, neno la Mungu linasema

Yeremia 17

5 Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana.

6 Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani palipo ukame, Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu.

7 Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake.

ukitaka kuijua kesho yako, mtegemee Mungu, Kwa kusoma neno huko ndiko utapata kuijua kesho yako

ubarikiwe

Pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Mafundisho zaidi, NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

LEAVE A COMMENT