Kujuzu ni nini ki- biblia 2wakorintho 12:4

Maswali ya Biblia No Comments

Neno hili kujuza maana ya yake ni kutoruhusiwa

tusome tuone Paulo alivyokuwa anaeleza jambo hili
2Wakorintho 12:2 “ Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu

3 Nami namjua mtu huyo, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua

 4 ya kuwa alinyakuliwa mpaka Peponi, akasikia maneno yasiyotamkika, ambayo haijuzu mwanadamu ayanene”

Hivyo hapo tunaona mitume Paulo, akieleza katika Maono yake jinsi alivyopelekwa juu mbingu ya tatu, lakini alisikia maneno ambayo akupewa ruhusa kuyasema watu

tunaweza ona tena neno hili katika kifungu hiki

Mwanzo 34: 7 “Wanawe Yakobo waliposikia hayo, wakaja kutoka nyikani; nao wakasikitika sana, wakakasirika mno, kwa sababu amefanya upumbavu katika Israeli kwa kulala na binti Yakobo, neno LISILOJUZU kutendeka”

Hivyo neno hili unapokutana nalo katika Biblia, maana yake ni KUTORUHUSIWA

Vivyo hivyo nasi katika wokovu wetu, yapo mambo au vitu ambavyo havijuzu Kwa mkristo kutenda, mfano ulezi, wizi, usengenyaji, wivu, kiburi na mambo yafananayo na hayo, ni vizuri kujiweka katika hali ya usafi yaani utakatifu sawa sawa neno la Mungu linavyotuagiza

1 Yohana 1

5 Na hii ndiyo habari tuliyoisikia kwake, na kuihubiri kwenu, ya kwamba Mungu ni nuru, wala giza lo lote hamna ndani yake

6Tukisema ya kwamba twashirikiana naye, tena tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatuifanyi iliyo kweli;

hivyo Kwa kuwa tupo nuruni basi Kuna mambo ya ulimwengu huu hayajuzu kuyatenda

Bwana akubariki.

Pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Mafundisho zaidi, NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *