Kuhusuru ni nini Ki-biblia ( luka19:43)

  Biblia kwa kina

Kuhusuru ni kitendo cha kuzingira kitu pande zote, kisiwe na mpenyo wa kutoroka au kupita

Na mbinu hizi mara nyingi zilitumika katika kipindi cha agano la kale, majeshi ya zamani wakati wa vita, walikuwa wana hususuru kwanza (kuzingira) maadui zao kabla hawajapigana ili wakose mpenyo au nafasi ya kuweza kutoka, na hii ilikuwa inachukua hata miezi, Hadi pale chakula kinapowaaishia, Sasa hali hiyo iliwapelekea hao maadui kutoka ili kutaka Amani au kupigana vita

Neno hili unaweza kukutaka nalo katika baadhi ya vifungu katika biblia

2 Wafalme 6:24-25

[24]Ikawa baada ya hayo, Ben-hadadi mfalme wa Shamu akakusanya majeshi yake yote, akakwea akauhusuru Samaria.

[25]Njaa ikawa kuu huko Samaria; na tazama, wakauhusuru, hata kichwa cha punda kikapata kuuzwa kwa vipande themanini vya fedha, na kibaba cha mavi ya njiwa kwa vipande vitano vya fedha.

1 Samweli 23:8

[8]Basi Sauli akawaita watu wote waende vitani, ili waishukie Keila, na kumhusuru Daudi na watu wake.

1 Wafalme 8:37

[37]Ikiwa nchi imeingia njaa, au tauni, au ukosefu wa mvua, au ukungu, au nzige, au panzi; ikiwa adui wamewahusuru katika nchi ya miji yao; au ukiwapo msiba wo wote, au uele wo wote;

Luka 19:43

[43]Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande zote;

Soma pia Kumbukumbu 20:12, 19, 2Wafalme 24:11, Isaya 29:4

Na jambo hili ndilo shetani analolitumia hata sasa katika Roho, pale anapotaka kuwadondosha watu mara nyingi uhusuru sehemu au nyezo ambazo ndizo huwa sehemu ya kuendeshea maisha yao mfano biashara kazi nk akishaona amezingira ndipo hapa ananza kutoa mawazo yake
Kwa kukulazimisha kufanye dhambi ili upate kitu

mfano unakuta mtu amefungiwa duka, na ili lifungulie analazimishwa kutoa rushwa ndipo afunguliwe duka lake, Sasa lazima tujue kuwa shetani ndivyo anavyofanya… ni kuwa makini.

Ndiyo maana hata tunajifunza Kwa Bwana wetu Yesu Kristo, pale ambapo shetani alijaribu kumshawishi ageuze jiwe kuwa mkate, jibu la Yesu lilikuwa la ujasiri alimwambia tu wake..akamwambia mtu hataishi kwa mkate, bali kwa kila Neno linalotoka katika kinywa cha Bwana.

Hii ikupe nawe ujasiri kuwa unapopitia changamoto yoyote na shetani anajaribu kukuletea vitu ufanye hili tu umkosee Mungu, wewe hupaswi kutishika bali, ni wakati wa kumwonyesha adui kuwa siishi kwasababu ya kitu hicho tu, bali naishi kwa Neno linalotoka katika kinywa cha Bwana, kupitia kufanya hivyo utashangaa Mungu anakufungulia milango zaidi hata ya kile ulicho kuwa nacho

ubarikiwe, zaidi sana ikiwa bado ujaokoka wakati ni huu maana mitengo ya shetani huwezi kuishinda bila kuwa nguvu ya Yesu Kristo, Amua Leo mpe Yesu maisha yako nawe utakuwa huru

Pia Kwa Maswali, Maombezi au Msaada wowote Wasiliana nasi Kwa namba hizi
+225789001312/ +225693036618

Pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Mafundisho zaidi, NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema.

LEAVE A COMMENT