Chuo cha Vita cha Bwana ni nini?.

  Biblia kwa kina

Shalom!, Bwana Yesu asifiwe!.

Chuo cha vita cha Bwana ni moja ya vitabu vya Kihistoria ambacho kina rekodi matukio yote ambayo Bwana aliwapigania watu wake na kuwashindia. Hivyo ni kitabu kinachoelezea matendo makuu ya Bwana alivyo wapigania na kuwashindia katika vita.

Kitabu hiki kimetajwa katika.

Hesabu 21:13 “Kutoka huko wakasafiri, wakapanga upande wa pili wa Arnoni, ulio jangwani, utokao katika mpaka wa Waamori; maana, Arnoni ndio mpaka wa Moabu, kati ya Moabu na Waamori.

14 Kwa hiyo imesemwa katika CHUO CHA VITA CHA BWANA, Wahebu katika Sufa, Na bonde za Arnoni,”

Ni kitabu ambacho hakijawa wazi hata leo na wala hakijawekwa katika Orodha ya vitabu 66 vilivyo kwenye Biblia Takatifu.

Na vitabu vingine vilivyotajwa lakini havijawekwa katika Biblia ni kama kitabu cha Samweli mwonaji. (1 nyakati 29:29), kitabu cha Wafalme cha Yuda( 1 Wafalme 14:29),kitabu cha tarehe ya Gadi mwonaji..

KITABU HIKI HAKIKO KWENYE BIBLIA?.

Biblia isingeliweza kurekodi kila kitu Mungu alichokifanya kwa kuweka vitabu visingelitosha… Kama Biblia inatuambia mambo tu aliyoyafanya Bwana Yesu yasingelitosha kwenye vitabu vyote na Alifanya kazi kwa muda wa miaka mitatu tu.

Hivyo Mungu ameona Habari hizo zilizo kwenye Biblia Takatifu kwa wakati wetu huu tulionao na vitatusaidia kama tukitia  nia na Roho Mtakatifu atatusaidia. 

Hivyo kwa habari hizo chache tuzisome lakini cha ajabu watu ni hatutaki kusoma yaani
Tumekuwa wavivu wa kusoma biblia Mungu atusaidie sana.

Kusoma ni jambo la msingi sana na ndio hata Paulo anamsisitiza Timotheo asiache kusoma atie bidii.

1Timotheo 4:13 “Hata nitakapokuja, ufanye bidii katika kusoma…”

Maran atha!.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

LEAVE A COMMENT